Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali
katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti 2016 imefanikiwa kulipa
jumla ya sh. bilioni 511.86 ikiwa ni malimbikizo ya mwajiri kwa
watumishi waliostaafu.
Hayo
yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji
alipokuwa akijibu swali la Mary Chatanda Mbunge wa Korogwe Mjini
aliyehoji kuhusu changamoto inayowakabili wastaafu ya kucheleweshewa
mafao yao na Mfuko wa pensheni wa PSPF katika mwaka wa fedha 2015/2016.
“Kucheleweshwa
kwa malipo ya wastaafuhakutokani na Serikali, isipokuwa waajiri ndio
baadhi ya nyaraka zinazohusika ili kuaandaa malipo ya wastaafu hao
alisema Dkt. Kijaji.
Naibu
Waziri Dkt. Kijaji amesema kuwa nyaraka zinazomhusu mtumishi
ziwasilishwe ndani ya muda wa miezi mitatu hadi sita kabla ya muda wa
kustaafu ili malipo yake yaweze kuandaliwa kwa wakati na kupata stahili
zao ili waweze kukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Aidha,
jumla ya sh. bilioni 83.25 zimelipwa ikiwa ni malipo ya deni kabla ya
mwaka 1999 hali inayoonesha kuwa Serikali inaendelea kulipa malimbikizo
ya madai ya wastaafu na mafao mengine yanayotolewa na Mfuko huo ili
waweze kuendesha maisha yao baada ya kustaafu.
Katika
kipindi cha mwezi Januari hadi Julai 2016 Mfuko umelipa mafao ya
pensheni ya mwezi kwa kiasi cha sh. bilioni 117 ambapo kwa sasa mfuko
huo unaendelea kulipa malimbikizo ya mafao ya mkupuo kwa wastaafu wapya
na mafao mengine.
Katika
kudhihirisha dhamira hiyo ya kulipa mafao ya wastaafu, Dkt. Kijaji
amesema kuwa tangu Julai 2015 bodi za mifuko ya hifadhi za jamii
zinaendelea kufanyia kazi mafao ya wastaafu na kuwalipa stahili zao kwa
asilimia 50 kulingana na maelekezo ya Serikali.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama ameliarifu Bunge kuwa mfumo
na sheria vimeunganishwa na kutoa fursa kwa mtumishi anapohama kutoka
ajira moja kwenda nyingine anaruhusiwa kuhama kutoka mfuko moja kwenda
mfuko mwingine.
0 comments:
Post a Comment