WATANZANIA zaidi ya asilimia 70 wamepewa
kipaumbele kushiriki katika shughuli za
kujenga uchumi wa nchi kufikia uchumi wa kati katika kutekeleza sera ya
uwezeshaji wananchi kiuchumi mpaka kufikia mwaka 2020.
Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la
Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi. Beng’i Issa wakati wa ufunguzi wa ripoti
ya Tathimini ya Sera ya uwezeshaji
wananchi kiuchumi ambao umefanyika leo jijini Dar es salaam.
“Tunataka kufikia 2020 watanzania asilimia zaidi
ya 70 waweze kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kufikia katika uchumi wa
kati ili kutekeleza sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi nchini” amesema Bi.
Issa.
Aidha Bi.Issa amesema kuwa watanzania wanatakiwa
washiriki katika shughuli za kiuchumi na wasitegemee zaidi wawekezaji kutoka
nje ili kuifanya Tanzania iendelee kiuchumi kutoka ngazi ya mmojammoja hadi kufikia maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa Meneja wa Utafiti na ufatiliaji wa
Sera hiyo kutoka NEEC Bi. Frola Kajela amesema kuwa Serikali imeandaa sera hiyo
ili kuwezesha watanzania kutumia rasilimiali zilizopo katika kuinua uchumi wa
nchi na kuweza kumilikiwa na watanzania wenyewe.
“Sera hii inalenga zaidi kwa watanzania kumiliki
uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini ili kujishughulisha
katika kuleta maendeleo ya nchi kwa jamii na taifa kwa ujumla mpaka kufikia
2020” alisema Bi. Kajela.
Aidha Bi. Kajela amesema kuwa sera hiyo inafanyiwa
maboresho ili kuweza kuwafikia watanzania wote katika kuelewa na kumiliki
uchumi kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza
mpango wa serikali uliyowekwa kuhakikisha watanzania wanajiinua
kiuchumi.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment