Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Hamisi
Kigwangalla akipokea maelezo kutoka kwa wataalam wa MEWATA juu ya zoezi
hilo.
Rais
wa MEWATA, Dkt Serafina Baptist Mkuwa akimpa maelezo Naibu Waziri wa
Afya Dk. Kigwangalla wakati akizunguka kukagua maeneo ya ukaguzi wa
upimaji huo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Hamisi
Kigwangalla akipokea maelezo kutoka kwa wataalam wa MEWATA juu ya zoezi
hilo.
Zoezi hilo likiendelea
Dk. Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na Madaktari wa MEWATA katika tukio hilo.
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha zoezi hilo la upimaji wa Afya bure linaloendelea katika Hospitali ya Peramiho.
Dk. Kigwangalla akitoa maelezo wakati wa ukaguzi wa zoezi hilo kwa kituo cha Hospitali ya Paramio.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Hamisi
Kigwangalla mapema jana Agosti 24,2017, amezindua rasmi zoezi la upimaji
wa Afya bure kwa akina mama linalofanyika kwa siku tatu kwenye uwanja
wa Majimaji na maeneo mengine ya Songea Mkoani Ruvuma.
Zoezi
hilo linaratibiwa na Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kwa
ushirikiano na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto na Serikali ya Mkoa wa Ruvuma. Kampeni itahusisha upimaji wa
Saratani ya Matiti, Saratani ya Shingo ya Kizazi, Kisukari, Shinikizo la
damu (Hypertension), Magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza na Ugonjwa
mengine yakiwemo ya kuambukiza (Kifua Kikuu).
Dk.
Kigwangalla aliwashukuru MEWATA, kwakuwezesha zoezi hilola upimaji Afya
bure ambapo zoezi hilo linaonyesha dhamira ya kuhakikisha kwamba jamii
ya Kitanzania inahamasika katika kupunguza tatizo la saratani kwa
ujumla, hususani saratani ya matiti na mlango wa kizazi na matiti.
“Nilipopata
mwaliko huu wa kuwa mgeni rasmi katika zoezi hili wala sikusita kabisa,
nilikubali kwa vile ninafahamu tatizo la saratani kwa wanawake nchini,
na mimi pamoja na Waziri wangu Mhe. Ummy Mwalimu ni wakereketwa wakubwa
wa Afya ya mama na mtoto, hivi hatutasita kushirikiana na mtu yeyote
mwenye nia njema hususan kwenye eneo hili, hapa Nchini kwetu, kwa ajili
ya kupunguza vifo vya mama na mtoto na vitokanavyo na saratani.”
Alieleza Dk. Kigwangalla.
Dk.
Kigwangalla amebainisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwamo
saratani, kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa sugu ya mfumo wa hewa,
magonjwa ya figo, seli mundu, na magonjwa ya akili, kwa sasa yamekuwa
yakiongezeka kwa kasi kubwa duniani kote na hapa nchini pia. Magonjwa
haya huchangia zaidi ya asilimia hamsini ya mzigo wa magonjwa duniani
kwa vile husababisha gharama kubwa za matibabu, ulemavu na hata vifo.
“
Tanzania na nchi nyingine kusini mwa Jangwa la Sahara zina viwango vya
juu vya saratani ya matiti na mlango wa kizazi. Nchini Tanzania, katika
saratani zinazo wapata zaidi wakina mama, saratani ya mlango wa kizazi
inaongoza ikifuatiwa na saratani ya matiti. Saratani hizi mbili kwa
pamoja husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya wakina mama
vitokanavyo na saratani.
Takwimu
katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha kuwa saratani ya
mlango wa kizazi ndiyo inayoongoza kwa asilimia 36% (zaidi ya theluthi
moja) ya wagonjwa wote wanaohudhuria katika taasisi. Aidha, mnamo mwaka
2005, kulikuwa na wagonjwa wapya 2500, ukilinganisha na wagonjwa wapya
5200 mwaka 2016. Hii inaonyesha dhahiri kuwa wagonjwa wameongezeka kwa
asilimia 100% kwa kipindi cha miaka 10. Idadi hii ni kubwa sana, hivyo
juhudi na ushirikiano zaidi zinahitajika katika kupunguza vifo hivi kwa
kushirikiana na taasisi na mashirika binafsi kama MEWATA na wengine
katika kutoa huduma za uchunguzi wa awali na matibabu.” Alieleza Dk.
Kigwangalla wakati akihutibia wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye
uzinduzi huo.
Akielezea
kuhusiana na tatizo la kisukari, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa,
tafiti za ugonjwa wa kisukari zinaonyesha kuwa mwaka 2007 kulikuwa na
wagonjwa 246 milioni duniani. Takwimu za mwaka 2015 kutoka kwenye Atlas
ya kimataifa ya Kisukari, zinaonyesha kuwa kulikuwa na wagonjwa milioni
415 duniani kote. Ifikapo mwaka 2040 inatarajiwa kuwa na wagonjwa
milioni 642.
“Katika
bara la Afrika kulikuwa na wagonjwa wa kisukari milioni 14.2 mwaka 2015
na idadi hii itaongezeka na kufikia milioni 34.2. Kwa Tanzania mpaka
mwaka 2015 kulikuwa na jumla ya wagonjwa 822,880 wa kisukari. Utafiti
uliofanyika mwaka 2012 na kuhusisha wilaya 50 nchini Tanzania ulionyesha
ya kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25-64 wana
ugonjwa wa kisukari. Hii inaonyesha ni jinsi gani ugonjwa wa kisukari
unavyoongezeka, na namna amabvyo mazoezi haya yatasaidia kwenye juhudi
za Serikali za kupambana na magonjwa haya.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
Kwa
upande wake, Rais wa MEWATA, Dkt Serafina Baptist Mkuwa, amewataka
wanawake mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo ili
kubaini tatizo mapema ili kuweza kuchukua hatua.
“Wananchi
wa mkoa wa Ruvuma na mikoa yote ya jirani, ni wakati mzuri wa kuitumia
vyema fursa hii muhimu, kuja kujichunguza afya zenu, na zoezi hili ni
bure kwa watu wote” alieleza Dk. Mkuwa.
Katika
tukio hilo pia lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Gosbert Mutayabarwa Wakuu wa Wilaya za Songea
Mjini na vijijini, Waganga Wakuu wa Wilaya, Wabunge wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akiwemo Mbunge wa Songea Mh, Gama, pamoja na
madiwani wote.
0 comments:
Post a Comment