Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NA DITHA NYONI WA RUVUMA TV
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amekanusha taarifa zilizozagaa
kwenye mitandao ya kijamii kuwa amepinga marafuku wananchi wa mkoa wa
Ruvuma wasiitane baby.
Tamko
hilo amelitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ikulu
ndogo ya mkoa wa Ruvuma , hii inakuja baadaya ya taarifa kuzagaa na
yenye picha inayoonesha mavazi tofauti na eneo alilokuwa anatoa ujumbe
katika shule ya sekondari NASULI na MBAMBA BAY huku ujumbe ukisomeka
“marukuku kuitana baby” mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
Hii ni picha inaonyesha tofauti na mazingira
Na hii ni picha inaonyesha eneo ambalo mkuu wa mkoa akizungumza na wanafunzi wa NASULI sekondari
Ikumbukwe
Novemba 8 mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Ruvuma alifanya ziara katika
halimashauri ya natumbo katika shule ya sekondari nasuli na kuzungumza
na wanafunzi hao, huku kampeni kubwa ili kuwa ni kueneza ujumbe wa
kumtaka mwanafunzi wa kike kuvaa maguni manne ambayo ni sare ya
shule,joho la maafari,gauni la harusi,na matreniti dress
“ili
muweze kufanikisha masomo yenu watoto wakike lazima mvae magauni ili
muweze kufanikisha malengo yenu”pia mkuu wa mkoa wa Ruvuma aliongeza
kuwa ni marafuku watoto wa kiume na wakike kuitana baby
“msikubali
kuitwa baby kwa sababu kukubali kuitwa baby ni chanzo cha kujiingiza
kwenye mapenzi,mskubali kuitwa queen we ni mwanafunzi unatafuta maisha
na wala usikubali kuitwa mrembo au mzuri alisema Rc MNDEME.
Lengo ya kampeni ni kumsaidia mwanafunzi wa kike aweze kufikia ndoto zake za kielimu na kuweza kufanikisha malengo yake.
Kufatia
taarifa hizo mkuu wa mkoa alisema ilikuwa inawalenga wanafunzi wa kike
na sio watu wazima kwani taarifa zinazoenezwa na makundi ya watu
wachache zinalengo la kupotosha umma hivyo wakazi wa mkoa wa Ruvuma
wapaswa kupuuzia
Aidha
amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kutumia kauli mbiu hiyo ya magauni
manne ili iwe chachu kwa wanafunzi wa kike waweze kufanikisha ndoto
zake,kwani wanaofanya hivyo hawana nia nzuri wa watoto wa kike
0 comments:
Post a Comment