na Stephano Chitete, SongeaKADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Golden Sanga (Sanga One), ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa chama hicho wilaya ya Songea katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa habari juzi mjini hapa, Sanga alisema ameamua kugombea nafasi hiyo, ili kurudisha heshima ya chama hicho mjini hapa.Alisema kila kukicha mvuto wa chama hicho miongoni mwa jamii umekuwa ukipungua kutokana na matendo maovu yasiyokuwa ya kimaadili yanayofanywa na viongozi wake ambayo yamekuwa yakiwakatisha tamaa wananchi na wanachama wa chama hicho.Alieleza kuwa hali hiyo imesababisha kata 6 kati ya 21 kuchukuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.Alieleza...
ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOANI RUVUMA WAKUTANA

Askofu mkuu wa jimbo la mbinga mkoani Ruvuma John Ndimbo akizungumza wakati wa kikao cha siku moja cha kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Ruvuma kilichofanyikas jana mjini mbinga kilicholengo kuwakumbusha wajibu wao askari hao baada ya kulalamikiwa na jamii juu ya kujihusisha na vitendo vya rushwa kunakosababisha kutokea ajali za barabarani mara kwa mara hapa nchini,katikati ni kamanda wa polisi wa cmkoa huo kamishina msaidizi wa polisi Deusidedit Nsimeki na kulia mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai(Rco) Revocutus Malimi.Kaimu kamanda wa taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa(Takukuru) wa mkoa wa Ruvuma Hamisi Kidulani akizungumza...
Local communities in Ruvuma Region urged to embrace Mkuju River Uranium Project

The Mantra Tanzania Community Relations Manager Benard Mihayo (right) stresses a point to the Ruvuma Region District Commissioners who were on a familiarilization tour at the Mkuju River Uranium Project site in Namtumbo District, Ruvuma Region at the weekend.
The Mantra Tanzania Geological Officer Roy Namgera (in white head gear) explains a point to Ruvuma Region District Commissioners who were on a familiarilization tour at the Mkuju River Uranium Project site in Namtumbo District, Ruvuma Region at the weekend. Second from the right (in red cap) is the Namtumbo District Commissioner Abdallah LutaviNamtumbo District Commissioner Abdallah...
Pinda: Jifunzeni kutoka kwa wawekezaji
Na Amon Mtega, SongeaWANANCHI wa Kijiji cha Lipokela, Kata ya Mbingamhalule wilayani Songea, wametakiwa kuacha kuwa watazamaji kwa wawekezaji na kufurahia fursa zao bali wafanye kazi ya kujifunza kutoka kwao.Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipotembelea shamba la kilimo cha kahawa la wawekezaji wa Kampuni ya Avivu Tanzania Ltd, lenye ukubwa wa ekari 1,934 lililopo kijijini wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Ruvuma.
Alisema kunufaika na wawekezaji waliopo, inatakiwa kushikamana nao zaidi kwa lengo la kujifunza namna ya utendaji kazi na hatimaye uchumi utakuwa kwa wote bila kuacha pengo kubwa kati ya mwekezaji na mwananchi mzawa.
“Msipofanya kazi hiyo ya kujifunza changamoto nyingi zitakuwa zinawakabili hasa suala la kipato ambacho huwa kinafikia mahali...
Mbinga kutumia ziwa Nyasa kuongeza mapato
Mussa Mwangoka, Mbinga-Ruvuma yetu
UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma umejiwekea mikakati kamambe ya kuongeza makusanyo ya halmashauri hiyo katika mwaka ujao wa fedha kwa kutumia vyema rasilimali zinazotokana na ziwa Nyasa na kuaanisha vyanzo kadhaa vya kukusanya kodi.
Akizungumza katika kikao cha pamoja baina Kamati ya Fedha na Wataalamu wa Halmashauri hiyo katika ziara yao ya siku nne mkoani Rukwa, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo , Oddo Kiliani Mwisho alisema kuwa wametumia muda mwingi kujifunza katika eneo la Ziwa Tanganyika mkoani Rukwa na kubaini dosari kadhaa zilizokuwa zikisababisha kupungua kwa pato la halmashari yao.
“Baada ya kufanya ziara mkoni Rukwa hususani katika maeneo ya...