Home » » SANGA KUWANIA UENYEKITI CCM

SANGA KUWANIA UENYEKITI CCM


na Stephano Chitete, Songea
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Golden Sanga (Sanga One), ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa chama hicho wilaya ya Songea katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi mjini hapa, Sanga alisema ameamua kugombea nafasi hiyo, ili kurudisha heshima ya chama hicho mjini hapa.
Alisema kila kukicha mvuto wa chama hicho miongoni mwa jamii umekuwa ukipungua kutokana na matendo maovu yasiyokuwa ya kimaadili yanayofanywa na viongozi wake ambayo yamekuwa yakiwakatisha tamaa wananchi na wanachama wa chama hicho.
Alieleza kuwa hali hiyo imesababisha kata 6 kati ya 21 kuchukuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.
Alieleza zaidi kuwa amejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na viongozi wenzake watakaochaguliwa kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama kukijenga chama na kuleta ushindi stahiki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2015.
Chanzo: Tanzania Daima



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa