Home » » ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOANI RUVUMA WAKUTANA

ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOANI RUVUMA WAKUTANA

Askofu mkuu wa jimbo la mbinga mkoani Ruvuma John Ndimbo akizungumza wakati wa kikao cha siku moja cha kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Ruvuma kilichofanyikas jana mjini mbinga kilicholengo kuwakumbusha wajibu wao askari hao baada ya kulalamikiwa na jamii juu ya kujihusisha na vitendo vya rushwa kunakosababisha kutokea ajali za barabarani mara kwa mara hapa nchini,katikati ni kamanda wa polisi wa cmkoa huo kamishina msaidizi wa polisi Deusidedit Nsimeki na kulia mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai(Rco) Revocutus Malimi.
Kaimu kamanda wa taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa(Takukuru) wa mkoa wa Ruvuma Hamisi Kidulani akizungumza jana wakati wa kikao cha siku mkoja kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wa mkoa huo,ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka askari hao kupunghuza malalamiko ya wananchi juu ya kujihusisha kwaio na vitendo vya rushwa vinavyopelekea kupindisha sheria za barabarani na kusababisha ajali nyingi hapa nchini.
Kamanda wa poisi mkoani Ruvuma kamishina msaidsizi wa poisi Deusidedit Nsimeki akizungumza na maafisa na askari wa kikosi cha usalama barabarani wa mkoa huo jana mjini wilayani mbinga,katika kikao cha siku moja cha kukumbushana wajibu wao hasa baada ya jamii kuwalalamikia askari hao kutokana na vitendo vya rushwa,kushoto mkuu wa wilaya ya mbinga Senyi Ngaga na kulia mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai(Rco) Revocutus Malimi.
Mmoja wa askari wa kikosi cha usalama bara barani mkoani Ruvuma aliyefahamika kwa jina moja la staff sajent Lilanga akichangia hoja wakjati wa kikao cha siku moja cha kukumbushana wajibu wa kazi kwa askari hao kilichoitishwa na kamanda wa polisi mkoani humo Deusidedit Nsimeki hayupo pichani kilichofanyika jana wilayani mbinga.
Mkuu wa wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma,Senyi Ngaga akifungua kikao cha siku moja cha kazi kwa maafisa na askari wa usalama barabarani wa mkoa wa Ruvuma kilichofanyika jjana wilayani humo,kulia kamanda wa polisi mkoani Ruvuma kamishina msaidizi wa polisi Deusdedit Nsimeki.
baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi mkoani Ruvuma wakimsikiliza kamanda wa polisi wa mkoa huo Deusdedit Nsimeki (hayupo pichani) jana wakati wa kikao cha kazi cha siku moja juu ya wajibu kikosi hicho0 hasa baada ya kutuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa vinavyosababisha kuongezeka kwa ajali nyingi hapa nchini.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii,Ruvuma.
Kwa hisani ya Michuzi blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa