Ruvuma
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania kanda ya Songea mkoani
Ruvuma imeanza vikao vyake katika vituo viwili tofauti Songea na Mbinga ambapo
kesi 37 za mauaji zitasikilizwa.
Msajili wa wilaya mahakama kuu Tanzania kanda ya
Songea Wilfred Nyansobera alisema kati ya kesi hizo zitakazosikilizwa zipo
ambazo maelezo ya awali na ushahidi utasikilizwa.
Nyansobera alisema kikao cha kwanza kitaendeshwa na
Jaji Patricia Fikirini akisaidiana na wakili mkuu mfawidhi wa serikali kanda ya
Songea Andikalo Msabila na wakili wa kujitegemea Christandus Komba na Frank
Ngafumika.
Alifafanua kuwa katika kikao hicho cha kwanza jumla
ya kesi 16 zimepangwa ikiwa 12 zitasikilizwa maelezo ya awali na nne
zitasikilizwa ushahidi.
Alisema kikao kingine kitaendeshwa na Hakimu Mkazi
Mkuu Wilfred Dyansobera akisaidiana na wakili wa serikali Okoa Mgavilenzi na
wakili wa kujitegemea Dickson Ndunguru ambapo kesi 10 zimepangwa ikiwemo nne za
wauaji kwa ajili ya kusikiliza ushahidi na sita rufaa za jinai.
Kikao kingine kinaendeshwa Mbinga na Jaji mfawidhi
kanda ya Songea Mwanaisha Kwariko ambapo jumla ya kesi 11 zimepangwa ikiwa kesi
tano za mauaji zitasikilizwa ushahidi na kwamba kesi tatu ni za rufaa za jinai
huku zingine tatu zikiwa ni maombi na rufaa ya kesi za madai.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment