Ruvuma
WAKULIMA wakorosho
wameitaka serikali na wadau wa sekta ya korosho nchini kushughulikia kero
zilizo katika mfumo wa soko la zao hilo ili liweze kumnufaisha mkulima na
kuongeza tija.
Hatua hiyo inatokana
na zao hilo kushindwa kutoa mchango stahiki kupunguza mzigo wa umaskini kwa
wakulima wa zao hilo linalotoa mchango mkubwa katika pato la taifa na kuingiza
fedha nyingi za kigeni.
Wakichangia mada ya
DHANA YA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI iliyowasilishwa katika mkutano wa wadau wa
sekta ya zao la korosho baadhi ya wakulima hao ndg Ally Maneno wa
Pwani,Nicodemas Wilson wa Lindi na Zainabu Kalikalanje wa Ruvuma wamesema swala
la upotevu wa korosho katika maghala ya wanunuzi ni changamoto kubwa ambayo
isiposhughulikiwa inakatisha tamaa wakulima.
Wamesema
kinachoendelea katika mfumo wa soko la korosho ambapo unyaufu unafikia asilimia
25 ya korosho zinazotunzwa katika maghala ni wizi ambao unsipoangaliwa utaua
sekta ya kilimo cha zao hilo hapa nchini.
Kumekuwepo na upotevu
wa korosho zinapokuwa katika maghala kusubiri bei ya soko mnadani ambao umekuwa
ukichukuliwa kama unyaufu madala ya upotevu ambao unepelekea wahusika
kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Kisayansi unyaufu
unaoruhusiwa katika zao la korosho ni kati ya asilimia 0.9 kwa kipindi cha
mwezi mmoja hadi asilimia 1 kwa kipindi cha miezi sita.
0 comments:
Post a Comment