TUME YA MIPANGO YATEMBELEA BANDARI YA MBABA BAY

Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba. Wengine kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje, Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Uongezaji Thamani Madini, Latifa Mtoro na Mwakilishi wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA), John Mvumula. Mfanyabiashara wa madini ya Shaba kutoka Kanda ya Kati Doreen Kisia, akisistiza jambo wakati akichangia hoja katika mkutano huo. Mmoja wa washiriki wa mkutano...

KAMPUNI YA MABATI YA ALAF YATOA MSAADA WA MABATI KWA AJILI YA UJENZI WA MAABARA ZA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA MBEYA.

 Meneja wa Kampuni ya ALAF Tawi la Mbeya, Greyson Mwakasege akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya kabla ya kumkabidhi msaada wa mabati 384 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara.  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King, akitoa shukrani kwa kampuni ya ALAF  kwa kujitolea mabati kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari za Wilaya ya Mbeya.   Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King na Meneja wa ALAF tawi la Mbeya, Greyson Mwakasege wakikabidhiana mabati 284 kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za Kata.  Mkuu...

SOMA HAPA-NANI ANACHEZESHA NGOMA YA ESCROW NA IPTL?

Kwa muda sasa kumekuwapo na tuhuma zinazohusu "wizi" wa fedha za akaunti ya escrow iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania mwaka 2006. Akaunti hiyo ilifunguliwa kwa ajili ya kuhifadhi fedha zilizokuwa zikilipwa na Shirika la Umeme Tanzania {TANESCO} kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL. Chimbuko la akaunti hiyo ni mgogoro wa tozo hiyo kwamba iligubikwa na utata baada ya kudaiwa kwamba Tanesco ilikuwa ikitozwa fedha nyingi kuliko inavyostahili.             Tuhuma za huo "wizi" hata hivyo hazikuishia tu kwa wahusika wakuu yaani makampuni ya umeme, bali zimetiririshwa hadi kwa watu binafsi ambao kimsingi hawana uhusiano wowote na mgogoro huo wa malipo na wala kuhusika kwa njia yoyote na hicho kinachodaiwa kwamba ni uporaji wa fedha...

MAHAKAMA YAAMURU MAITI IFUKULIWE

MGOGORO wakugombea Mwili wa mzee Cleophas Senga (80) Mkazi wa Chanji, Wilayani hapa, mkoani Rukwa, umechukua sura mpya baada ya Jeshi la Polisi kufukua maiti ya mzee huyo kwa amri ya Mahakama na kuihifadhi katika hospitali ya hospitali ya Mkoa wa Rukwa. Maiti hiyo ilifukuliwa jana, majira ya saa 4:40 asubuhi katika makaburi ya Mandela, huku baadhi ya mitaa mjini hapa ikisimamisha huduma za biashara kwa muda wakati umati wa watu ukiwa umejitokeza kushuhudia tukio hilo. Baadhi ya akinamama waliojitokeza kushuhudia zoezi la ufukuaji wa maiti hiyo waliangua kilio baada ya kuona maiti ikitolewa kaburini na kuingizwa katika gari la polisi aina ya Toyota Landcruiser lenye namba za usajili PT 1275. Akiongea na mwandishi wa habari, mdogo wa marehemu, Dominiki Senga, alisema mgogoro huo umetokana...

MAJEMBE WAILALAMIKIA MANISPAA YA SONGEA

KAMPUNI ya Majembe Auction Mart imeilalamikia halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kwamba haijatoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya ulipaji wa ushuru (Service Levy), kabla kampuni hiyo haijaanza kazi ya ukusanyaji. Majembe Auction Mart imeingia mkataba na manispaa hiyo kuwa wakala wake wa ukusanyaji ushuru. Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Majembe Auction Mart Nyanda za Juu Kusini, Nelson Mwasomola, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, baada ya wafanyabiashara wa manispaa ya Songea kuituhumu kampuni hiyo kuwa wanatumia nguvu katika ukusanyaji wa ushuru ambao wenyewe hawajapewa elimu juu ya ulipaji huo. Mwasomola, alisema kuwa wafanyabiashara wana haki ya kulalamika, kwa sababu halmashauri ilitakiwa iitishe mkutano wa kuwatambulisha kabla ya kuanza kazi...

WANASHERIA MWANZA WAIFAGILIA WINDHOEK WASEMA NI BORA KWA AFYA

 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira akizungumza katika hafla fupi iliyowashirikisha baadhi ya wanasheria wa jiji la Mwanza kujadili bia za windhoek pamoja na maendeleo ya jiji hilo. Halfa hiyo ilikwenda sanjari na kila mgeni mualikwa kuchangia mada.  Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira (katikati), akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mmiliki wa  The Joint Pub iliyopo Isamilo jijini Mwanza.  Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira (kulia), akisisitiza jambo  katika hafla hiyo. Kulia ni Mmiliki wa  The Joint Pub, iliyopo Isamilo jijini Mwanza. (Imeandaliwa...

MWANZA WAIKUBALI WINDHOEK WAFURAHIA MPANGO WA KIWANDA CHA MABIBO BIA WA KUJENGA KIWANDA

Chupa za Windhoek zinavyoonekana.  Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira akizungumza na wadau na wanahabari wa jiji la Mwanza wakati wa Promosheni ya Bia za Windhoek iliyofanyika leo usiku katika Hoteli ya Villa Park Resort jijini humo.  Mshauri Mkuu wa Fr James Rugemalira, Aniki Kashasha akizungumza na wadau wa jiji la Mwanza pamoja na wanahabari kuhusu bia za windhoek Lager na Windhoek Draught.   Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira (katikati), akiwa amekaa na viongozi mbalimbali meza kuu. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni inayosambaza Gas ya Oryx jijini Mwanza...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa