Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya kumchoma moto Sofia Mwingira (34), katika mtaa wa Luseteni wilayani Namtumbo.
Wanaoshikiliwa ni mhudumu wa afya wa hospitali ya Wilaya ya Namtumbo, Nia Kilawi na dereva pikipiki ‘bodaboda’.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi (ACP), Mihayo Msikhela, tukio hilo lilitokea Oktoba 22 ambako waliukuta mwili wa marehemu umechomwa moto na kuteketea kuanzia kwenye mapaja hadi kifuani.
Alisema uchunguzi wa daktari ulibaini kuwa, marehamu hakuuwawa kwa kuchomwa moto bali alichomwa wakati ameishauwawa kutokana na mazingira walivyoukuta mwili ulivyolala.
Alisema kikawaida, mtu anayekufa kwa kuchomwa moto lazima atajihangaisha tofauti na walivyokuta amelazwa kama gogo na kudhihirisha kwamba, walimleta eneo hilo akiwa ameshauwawa na kwamba, polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Daktari wa hospitali ya Wilaya ya Namtumbo, Dk. Simoni Chacha, alisema alimtuma msaidizi wake kwenda kuchunguza mwili wa marehemu na cha kushangaza walikuta ameungua kuanzia mapajani, kifuani pote mapafu na maini yote, hivyo hakukuwa na uwezekano wa kupima na kujua kilichomsibu.
“Unajua mtu anaye kufa kwa kuchomwa moto huwa anahangaika, unaweza kuona dalili za kutaka kujinasua lakini moto huu uliomuunguza huyu mama ni ajabu hakuna pilika zozote zilizoonyesha kuwa alihangaika na mahali hapo palikuwa nje sio ndani, labda unaweza kusema alishindwa,” alisema Dk. Chacha.
Inaelezwa kuwa pembeni mwa mwili wa marehemu, walikuta dumu la mafuta linalosadikika lilitumika kuwekea mafuta ya petroli, tochi pamoja na kitenge cha marehemu na kwamba, majirani walisema kuwa baada ya kumuua mtuhumiwa walimnywesha petroli mdomoni wakawasha kiberiti na kutumbukiza mdomoni na moto ukalipuka.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment