Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JAMII imeshauriwa kutumia fursa zinazopatikana kwenye taasisi za fedha, benki na nyinginezo kujipatia mikopo itakayowasaidia kujikwamua kimaisha.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Benki ya Posta (TPB), tawi la Songea, Joseph Shirima, wakati akizungumzia mafanikio ya Benki hiyo yaliyopatikana kwa miaka 13 tangu hudumu hiyo ianze kutolewa mkoani Ruvuma.
Shirima, alisema benki hiyo ni ya wananchi wa Tanzania kwa asilimia 100, kinachozalishwa, kinachopatikana kinabaki na kutumika na Watanzania, hivyo kila mwananchi anapaswa kuitumia kikamilifu kwa kuwa imelenga kuwainua wenye kipato kidogo, cha kati pamoja na wafanyabiashara wakubwa kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu.
“Benki ya Posta imejikita katika kutoa mikopo midogo na mikubwa kwa wafanyabiashara, vikundi na watu binafsi kwa wenye kipato cha chini, walio na dhamana na wale ambao hawana dhamana…
“Sisi tunaamini kwamba, kama watoa huduma ni lazima tuwe wa bei rahisi kwa wanaohitaji huduma kwetu, na hii ndiyo imani yetu tukisisitiza kuwa anayehitaji huduma awe wa ghari na thamani kwetu,” alisema Shirima.
Alisema hivi sasa wamepata mafaniko makubwa baada ya kuwaaminisha wananchi kuwa wapo tayari kutoa huduma bora, wamejitokeza kwa wingi kiasi cha kuongezeka mara dufu amana na mikopo imeongezeka mara tatu ya kiwango kilichokuwa kinatolewa awali.
Hadi sasa benki hiyo ina vikundi 25 vinavyonufaika na huduma za Benki ya Posta, ambao wanakopa kadiri ya hitaji lao, ingawa wanashauri kwa wateja wapya kuanza na kiwango cha chini.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment