Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Bondia Salum Nassoro akipasha na kocha wake, Maneno Abdallah katika gym yao iliyopo Mazense Midizini.
Promota wa mchezo huo, Haruna Musa katika picha ya pamoja na bondia, Salum Nassoro.
Kampuni
ya Dippo Boxing Promotion ya jijini Dar inayoongozwa na promota, Haruna
Musa imeandaa pambano la Uzito wa Kati ‘Middle Weight’ kati ya bondia
Salum Nassoro wa Dar na Benson Mwakyembe wa Ruvuma mchezo utakaopigwa
Siku Kuu ya Pasaka, Machi 28 mwaka huu.
Pambano
hilo la kukata...
BENKI YA POSTA TANZANIA YAJENGA VYOO VYENYE THAMANI YA SH. MILIONI 4.7 KATIKA SHULE YA MSINGI MAKAMBI ILIYOPO MANISPAA YA SONGEA MKOANI RUVUMA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wanafunzi wa shule ya
msingi ya Makambi iliyopo Kata ya Ndilima Litembo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifurahia vyoo vya
kisasa vilivyojengwa na Benki ya Posta Tanzania.
Meneja Mwandamizi wa
Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akiongea kwenye mkutano katika shule hiyo muda mfupi kabla ya kuzindua vyoo hivyo.
Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua vyoo vyenye matundu 14, vitakavyohudumia...
SERIKALI KUSAMBAZA MADAKTARI BINGWA MAENEO YA PEMBEZONI IKIWEMO MKOA WA RUVUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akitoa ufafanuzi juu ya Wizara yake kuhakikisha itapeleka Madaktari bingwa katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo hospitali hiyo ya Mkoa wa Ruvuma wakati wa ziara yake aliyoifanya mapema Februari 13.2016.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto mjini Songea, Dkt. Hamisi Kigwangalla baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma na kituo cha afya cha Mjimwema kilichopo mjini Songea huku akiitaka...
KILWA YAAGIZA TANI 60 ZA CHAKULA CHA NJAA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
HALMASHAURI ya Wilaya Kilwa imeagiza tani 90 za mahindi mkoani Ruvuma kwa ajili ya kaya zilizoathiriwa na mafuriko.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Twaib Mbasha aliyasema
hayo alipozungumza na wajumbe wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana.
Alisema halmashauri imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo hilo.
“Gari liko njiani likitokea mkoani Ruvuma linalosafirisha mahindi kuletwa wilayani hapa,” alisema.
Mbasha alisema ni vigumu kuwaacha wananchi hivi hivi bila ya kutoa...
CCM YATAKA MAGUFULI AUNGWE MKONO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais Dk. John Magufuli.
Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Ruvuma kimewataka
wanachama wake kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dk. John
Magufuli, katika kupambana na ufisadi na kuwabana wakwepa kodi.
Rai hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo
Mwisho, wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi, wakiwamo wanachama wa
chama hicho kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM,
yaliyofanyika katika kata ya Subira, mjini hapa.
Mwisho...
WALIMU WATAKIWA KUCHAPA KAZI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako
BAADA ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini kufanya vibaya
katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2015 kwa kushika mkia
mkoani Ruvuma, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Sigsbert Kaijage
amewataka walimu kuongeza bidii katika ufundishaji ili kuondoa aibu
hiyo kubwa.
Mbali na hilo, Kaijage aliwataka wanafunzi, walimu, wazazi na walezi
wilayani humo kushirikiana ili kuinua kiwango...
WAKULIMA WA MAHINDI 'WAILILIA' SERIKALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKULIMA wa mahindi wilayani Songea mkoa wa Ruvuma, wameiomba
serikali kuongeza fedha kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA)
Kanda ya Songea ili wanunue mahindi mengi kwa msimu wa kilimo wa mwaka
2016/2017.
Wakulima hao walisema kutokana na hali ya hewa ya mwaka huu, hasa
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa wingi katika maeneo mkoani
Ruvuma, wana imani uzalishaji utakuwa mkubwa, ikilinganisha na msimu
uliopita.
Walisema ni vyema sasa serikali ikaanza kutafuta...