Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BAADA ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini kufanya vibaya
katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2015 kwa kushika mkia
mkoani Ruvuma, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Sigsbert Kaijage
amewataka walimu kuongeza bidii katika ufundishaji ili kuondoa aibu
hiyo kubwa.
Mbali na hilo, Kaijage aliwataka wanafunzi, walimu, wazazi na walezi
wilayani humo kushirikiana ili kuinua kiwango cha taaluma kwa lengo la
kufikia malengo ya Mpango maalum wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Kaijage alitoa mwito huo hivi karibuni wakati akizungumzia kufanya
vibaya kwa shule za halmashauri hiyo jambo lililoitia aibu kubwa kwa
kuwa ni mara ya kwanza Halmashauri ya Wilaya ya Songea kushika mkia.
Alisema iwapo kila mmoja kuanzia mtoto, mwalimu na mzazi watachukua
hatua stahiki na kila mmoja kutimiza wajibu wake itasaidia kufikia kwa
malengo yaliyoelekezwa na serikali badala ya jukumu hilo kuliachia
serikali.
Kaijage aliwataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kutumia
muda mwingi kwa ajili ya kujisomea na kuepuka kushiriki katika vitendo
vibaya vinayoweza kuchangia kukatisha ndoto za maisha yao.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment