Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) waikatalia halmashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kukatisha mkataba wa ujenzi wa ofisi za halmashauri hiyo,Hii ni baada ya Baraza la madiwani la halmashauri hiyo kukubaliana kwa pamoja na kustisha mkataba. Wasema kama halmashauri itasitisha mkataba itabidi halmashauri iwalipe fidia TBA.
NAIBU SPIKA MH. DKT TULIA ACKSON AKABIDHI HUNDI YA TSH MIL.8 KUCHANGIA UJENZI WA HOSPITALI WILAYA YA NAMTUMBO.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgeni
rasmi Mh. Dkt Tulia Ackson akinadi korosho katika harambee yauchangiaji wa
ujenzi wa hospitali ya Wilaya Namtumbo iliyofanyika jijini Dar es salaam
Mgeni
rasmi Mh Dkt Tulia Ackson na baadhi ya viongozi wakitazama makala fupi ya Ujenzi
wa Hospitali hiyo ilipoanza na baadhi yamajengo ya hospitali hiyo ya Wilaya ya Namtumbo
Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya Mantra Bw. Fredy Kibodya akielezea jambo kwa mgeni rasmi katika
harambee ya uchangiaji wa Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo
Mgeni rasmi
Mh Dkt Tulia Ackson akikabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi millioni nane kuchangia ujenzi wa hospital ya Wilaya ya Namtumbo
Mkuu wa wilaya ya namtumbo Bi. Luckness Alima akilia
kwa furaha baada ya kuchangiwa sehemu ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo.
RC RUVUMA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUSIMAMIA VYEMA MAADILI YA WAUMINI WAO
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amewataka viongozi wa dini mkoa
humo kusimamia vyema maadili ,unywaji pombe uliokithiri pamoja na
matumizi ya madawa ya kulevya
amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini katika ikulu ndogo
mjini songea
VIDEO:NAIBU WAZIRI WA UJENZI AMTAKA MKANDARASI KUMALIZA DARAJA KWA WAKATI
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu waziri wa ujenzi ELIAS KWANDIKWA amemwagiza mkandarasi anayejenga daraja la RUHUHU liliopo lituhi wilayani nyasa mkaoni ruvuma ambalo pia linganisha mkoa wa LUDEWA kukamilisha kwa wakati ili kupisha shughuli za maendeleo zinazofanywa na wananchi katika maneneo hayo.
Naibu waziri kwandikwa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja hilo na kuridhishwa na hali ya ujenzi unaofanya na kampuni ya lukolo HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE
VIDEO:RC RUVUMA AWAONYA WAFANYABIASHARA WA MBOLEA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma B CHRISTINA MNDEME amefanya ziara ya kushitukiza katika maghara ya SONAMCU ya kuhifadhia mbolea huku akikuta uchache wa mbolea katika maghara hayo habari kamili hii hapa video yake.

VIDEO:WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WA HALIMASHAURI YA WILAYA YA NYASA KUMALIZA TOFAUTI ZAO.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri mkuu wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania KASSIM MAJALIWA, amewaagiza viongozi wa halimashauri ya NYASA akiwemo mbunge wa jimbo hilo, mkuu wa wilaya na mkurugenzi, kumaliza tofauti zao na madala yake wawaletee wananchi maendeleo.
Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na watumishi na wakuu wa idara mbalimbali wa halimashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
VIDEO:WAZIRI MKUU AMEIAGIZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUUNDA CHOMBO KITAKACHOSIMAMIA MASUALA YA FUKWE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri mkuu KASSIM MAJALIWA ameiagiza wizara ya maliasili na utalii kuunda chombo kitakachomamia maeneo yenye fukwe, ili kulinda maeneo hayo yaweze kuvutiwa na watalii wakigeni wanaokuja katika maeneo hayo.
Waziri mkuu ameyasema hayo wakati wa kufunga tamasha la utalii lililofanyika MABAMBA BAY wilayani ya NYASA mkoani Ruvuma.
UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA SONGEA MJINI WAZIDI KUIMALIZA KAMBI YA UPINZANI
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Moses Machali akimnadi Dkt Damas Ndumbaro |
Wakati
kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo wa jimbo la Songea mjini mkoani
Ruvuma zikiendelea katika kata mbalimbali za manisipaa ya Songea mkoani
Ruvuma kwa ajili ya kumpata mbunge wa jimbo hilo ambaye chama cha
mapinduzi kimemteua Dkt Damas Ndumbaro kupeperusha bendera ya chama
hicho waliokuwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani nchini
wamezidi kujitokeza kwenye kampeni hizo na kutangaza kuachana na vyama
vyao vya awali.
Miongoni
mwa viongozi hao wa vyama vya upinzani ni pamoja na waliokuwa wajumbe
watatu wa serikali ya mtaa wa Majengo mjini Songea kwa tiketi ya chama
cha demokrasia na maendeleo ambao walitangaza uamuzi huo wa kukihama
chao hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi baada ya hotuba ya siku
mbili mfululizo kwenye kampeni hizo za kumnadi mgombea ubunge wa jimbo
hilo kwa tiketi ya chama cha mapinduzi iliyotolewa na aliyewahi kuwa
mwanachama wa chama na kingozi pia cha Demokrasia na maendeleo Moses
Machali.
Katika
hotuba yake ya kumnhadi mgombea huyo Machali alieleza sifa alizo nazo
mgombea Dkt Damas Ndumbaro ambazo alizifahamu muda mrefu tangu akiwa
kwenye kambi ya upinzani ambazo alisema hazina mashaka yoyote ya
kumfanya asichaguliwe kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo hilo na
kuwataka wananchi wa jimbo la Songea mjini kwa ujumla kuitokeza kwa
wingi siku ya Januari 13 mwaka huu kumpigia kura mgombea huyo na kuacha
kuendelea kusikiliza na kufuata propaganda za wagombea wa vyama vya
upinzani ambao walio wengi hawajui kilichoko kwenye vyama hivyo vya
upinzani kwa sababu yeye alikuwepo huko na anajua kulivyo.
Viongozi
wengine wa kambi ya upinzani waliopanda jukwaani katika viwanja vya
mikutano vya Majengo na kutangaza kujiunga na chama cha mapinduzi ni
pamoja na aliyekuwa katibu wa chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Kigoma
Sharon Msanya ambaye kabla ya kutangaza kujiunga na chama cha mapinduzi
aliwataka wapiga kura wa jimbno la Songea mjini kutokuthubutu kulifanya
jimbo hilo kuwa kambiya upinzani kwa sababu kufanya ni kurudisha nyuma
jitihada za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo ambayo
wameyahityaji kwa muda mrefu kurtoka serikalini na serikali ya awamu ya
tano inaendelea kuonesha dhamira ya dhati kuwafikishia wananchi
maendeleo hayo.
Alisema
yeye amekuwa kiongozi mkubwa wa chama cha ACT Wazalendo katika ngazi ya
mkoa lwa Kigoma akini amefikia uamuzi huo wa kusafiri kutoka mkoani
Kigoma mpaka mjini Songea ili aweze kupata fursa ya kuwaeleza wananchi
wa Songea umuhimu wa kukiunga mkono chama cha mapinduzi na mgombea wake
Dkt Dams Ndumbaro kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla kwa
sababu mgombea huyo amekuwa mpigania maendeleo ya taifa kwa muda mrefu
hata kabla hajafikia uamuzi huo wa kugombea nafasi hiyo ya kuwawakilisha
wananchi wa jimbo lake.
Huku
naye Edna Sunga aliyekuwa katibu wa kamati ya maendeleo ya jamii taifa
na mjumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu taifa wa chama cha ACT
Wazalendo akizungumza baada ya kukihama chama hico na kujijnga na chama
cha mapinduzi amesema kwa sababu yeye ni muumini wa kuzingatia miiko na
vita dhidi ya rushwa na kuwaletea maendeleo wananchi ameona hana sababu
ya kuendelea kuwa kwenye upinzani badala ya kuongeza na kujnganisha
nguvu ya kuwajhudumia wananchi walio wengi.
Amesema
kiongozi au mwananchi yeyote mwenye dhamira ya dhati ya maendeleo
ambayo wananchi walio wengi wanayahitajihana budi kukiunga mkopno chama
cha mapinduzi na mgombea wake ambaye amevaa taswira ya chama hicho na
taifa kwa ujumla huku naye mgombea wa jimbo hilo kwenye uchaguzi huo
akiendelea kuwaomba wananchi wa mji wa Songea kujiktokeza kwa wingi siku
hiyo ya uchaguzi kwa ajili ya kupiga kura kwa chama cha mapinduzi.
Na Nathan Mtega, Jamvi la habari - Songea
MHASIBU HALMASHAURI YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA AJISHINDIA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 ZA TATUMZUKA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mh.Luckiness Amlima akimkabidhi
mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 50 Mkazi wa wilaya ya
namtumbo mwenye umri wa miaka 31,ambaye ni Mhasibu msaidizi wa
halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma,ndugu Jacob Ndee
aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 50 .
Akielezea
kwa furaha za kushinda kitita cha milioni 50 za mchezo huo wa
kubahatisha wa TatuMzuka,Jacob alisema kuwa ndoto yake kubwa siku
akipata fedha za kutosha atazitumia kwa Kilimo,Anasema kwa sasa anaona
ndoto yake imetimia baada kupata fedha hizo,hivyo atazitumia katika
kilimo.
Mkuu
wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mh.Luckiness Amlima akiwa katika
picha ya pamoja na mshindi wa Kitita cha Milioni 50 cha TatuMzuka Ndugu
Jacob Ndee pamoja na baadhi ya Wadau wengine,ambapo pia walionekana
kuuufurahia ushindi wa Jacob,ambaye ni Mhasibu msaidizi wa
halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma.
Dkt KALEMANI akagua maeneo ambayo Waziri Mkuu ataweka Jiwe la Msingi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametembelea maeneo mawili
anayotarajiwa kuwekewa jiwe la msingi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tarehe 7/01/2018 katika wilaya
ya Songea mkoani Ruvuma.
Mradi wa kwanza aliotembelea ni wa jengo la Tanesco Mkoa wa Ruvuma lililoanza kujengwa mnamo mwaka 2014 ambao ulitarajiwa kukamilika mwishaoni mwa mwaka jana na kushindikana kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Mkandarasi.
Aidha mradi wa jengo hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu na kuanza kutumika rasmi.
Pamoja na kutembelea jengo hilo la Ofisi ya Tanesco Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Kalemani alitembelea eneo kunakojengwa mitambo ya kupoozea umeme katika mradi mkubwa wa kusafirisha umeme wa Makambako Songea uliopo wilayani Songea mkoani Ruvuma ambako alijadiliana na wataalamu na kuweka baadhi ya vitu sawa tayari kwa ajili ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi. Meneja wa Mradi Mkubwa wa Usafirishaji wa Umeme wa Makambako - Songea Mhandisi Didas Lyamulya akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipotembelea eneo la ujenzi wa mitambo ya kupoozea umeme unaoendelea kujengwa wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirirka la Umeme Tanzania (Tanesco) akieleza jambo mbele ya wajumbe walioambatana na Waziri wa Nishati ili kukagua eneo litakalowekwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika eneo la ujenzi wa Mitambo ya Kupoozea Umeme katika mradi wa Kusafirisha umeme wa Makambako Songea.Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto ) akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme katika mradi wa Kusafirisha Umeme wa Makambako-Songea wilayani Songea tayari kwa ajili ya kuwekwa kwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho Tarehe 7/01/2018.Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania Dkt. Tito Mwinuka akimweleza jambo walipotembelea eneo la uzinduzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa Makambako-Songea ili kujionea maandalizi ya uzinduzi huo.