Songea
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimike ametoa onyo kwa kiongozi yeyote atakayewatumia Wanafunzi kama chombo cha kutetea maslahi ya Walimu na kuunga mkono mgomo huo.
Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake, alisema kuwa mwalimu atakaye onekana kuwashawishi wanafunzi kushiriki maandamano kwa lengo la kuwatetea walimu atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kamanda Nsimike alisema kuwa baadhi ya walimu mkoani humo wamejiingiza kwenye mgomo huo kwa shinikizo kutoka kwa viongozi wao na kwamba baadhi ya walimu wameanza kutumia Wanafunzi kuwa kisemeo chao kwa kuishutumu serekari na kuitaka iwape masilahi walimu.
Aliwataka Viongozi wa CWT kutokwenda shuleni kuwashawishi Waalimu kujiunga na mgomo kwa kusambaza nyaraka au kuwashawishi kwa mdomo vinginevyo watakamatwa kwa makosa ya kukiuka amri hiyo.
Mkoa wa Ruvuma umekuwa mmoja wapo uliounga mkono mgomo wawalimu ambapo ni shule za watu binafsi pekee ndio ambazo hazijashiriki mgomo huo.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment