MKUTANO MKUU WA TATU WA PSPF WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Rais mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akizindua huduma mpya ya PSPF Pamoja nawe na PSPF call centre, itolewayo na mfuko wa Pensheni wa PSPF, baada ya kufungua Mkutano mkuu wa tatu wa wadau wa mfuko huo Feb 26.2014.  Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Hassan Mwinyi, kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, kulia kwake ni Ndugu Peter Ilomo aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF George Yembesi, Mkurugenzi Mkuu PSPF, Adam Mayingu na Katibu Mkuu MPAIC,...

MHAGAMA ; TEHAMA ITAONDOA TATIZO LA WALIMU, VITABU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  WADAU wa elimu wamekubali kutumia teknolojia ya habari na mwasiliano kufundisha na kujifunza ili kukabili tatizo la uhaba wa walimu na vitabu linalokwaza maendeleo ya elimu nchini. Hayo ni baadhi ya maazimio yaliyotokana na mjadala wa siku mbili wakati wa kongamano la elimu ulioandaliwa na Taasisi ya Learning InSync International kwa kushirikiana na British Council na kufanyika mjini Moshi, Kilimanjaro. Akizungumza kwenye kongamano hilo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama, alisema ili kuharakisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano...

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA WADAU WA PSPF

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA WADAU Mfuko wa Pensheni wa  PSPF unatangaza kwamba kutakuwa na Mkutano Mkuu wa tatu wa wadau utakaofanyika tarehe 26 na 27  Februari 2014 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo barabara ya Shaban Robert  jijini Dar es salaam. Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na changamoto zinazokabili Mfuko na sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla. “PSPF - TULIZO LA WASTAAFU” Mkurugenzi Mkuu Mfuko...

Kichanga kilichotupwa kipo hai

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  HUYU ni mtoto aliyetupwa na mama yake mara baada ya kujifungua katika eneo la Mkuzo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma hivi karibuni.Mama mzazi wa mtoto huyo anadaiwa kumtupa huku amemuhifadhi ndani ya mfuko kisha yeye kukimbia.Wasamaria wema walimuokota mtoto huyo akiwa hai na kumpeleka katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma HOMSO  ambako anaendelea kulelewa na kupata huduma zote muhimu kwa mtoto mchanga. Wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma  wamempa jina la Thomas huku wakiendelea...

RC RUVUMA AWATAKA POLISI KUFUATA MAADILI YA KAZI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said thabit Mwambungu amelitaka jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma kufuata Maadili na kuheshimu Kanuni, Taratibu na Sheria za Nchi                    Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ameyasema hayo wakati Jeshi la Polisi lilipofanya Maadhimisho ya kuukaribisha mwaka 2014 Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) sherehe zilizotanguliwa na paredi la Kikosi cha kutuliza ghasia. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema Kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kulinda mali za raia pamoja na kutii mamlaka yaliyopo katika Dola kinyume na hapo nikulidhalilisha jeshi la Police kimaadili. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema sifa ambayo...

Adaiwa kumuua mwanawe kwa kumbamiza kwenye lami

Mkazi  wa kijiji cha Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, Onestory Mgaya (31), ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumuua mtoto wake mwenye umri wa miaka saba kwa kumbamiza  kwenye barabara ya lami. Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Deusdedit Nsimenke, alimtaja mtoto aliyeuawa kuwa ni  Nesta Mgaya. Kamanda Nsimenke alisema tukio hilo lilitokea Februari 9, mwaka huu saa 5:00 asubuhi katika kijiji cha Lilondo wilayani Songea. Alifafanua kuwa inadaiwa kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa huyo, mkewe, Blesila Mponda (30)  na mtoto wao Nesta, walitoka Madaba kwenda kijiji cha Lilondo kusalimia wazazi. Hata hivyo, alisema wakiwa njiani kurudi nyumbani kwao,mkewe Blesila alibaini kuwa amesahau kadi ya kliniki ya mtoto wao na hivyo akalazimika kumuachia mumewe mtoto huyo ili...

Polisi 14 nguvuni kwa kuiba mali ya Sh900 mil

Polisi mkoani Ruvuma, wameingia katika kashfa, baada ya askari wake kutuhumiwa kuiba vitu vyenye thamani ya zaidi ya Sh900 milioni waliyokuwa wakivilinda. Vitu hivyo ni mali ya mkandarasi aliyefukuzwa katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Namtumbo hadi Tunduru. Tayari polisi 14 wamesimamishwa kazi na wanasubiri kuvuliwa magwanda ili kufikishwa mahakamani. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimike, jana alithibitisha habari hizi kwa njia ya simu. Alisema tukio hilo limelifedhehesha Jeshi la Polisi na kwamba taratibu za kuwafukuza kazi askari hao zinaendelea kabla ya kufikishwa katika vyombo vya sheria. Mtoa habari wetu alisema kashfa hiyo iligundulika mwezi uliopita,...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa