Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
HUYU
ni mtoto aliyetupwa na mama yake mara baada ya kujifungua katika eneo
la Mkuzo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma hivi karibuni.Mama mzazi wa
mtoto huyo anadaiwa kumtupa huku amemuhifadhi ndani ya mfuko kisha yeye
kukimbia.Wasamaria wema walimuokota mtoto huyo akiwa hai na kumpeleka
katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma HOMSO ambako anaendelea
kulelewa na kupata huduma zote muhimu kwa mtoto mchanga.
Wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma wamempa jina la Thomas huku wakiendelea kutoa malezi bora kwa mtoto huyo ambaye alizaliwa akiwa na uzito pungufu.Hata hivyo mtoto anaendelea vizuri katika wodi ya wazazi na uzito wake unaongezeka .Hapana shaka mtoto Thomas akitimiza uzito unastahili anaweza kwenda kulelewa katika vituo vinavyolea watoto yatima kama vile kituo cha kulelea yatima cha watawa wa mtakatifu Agnes Chipole Songea.
Tabia ya wasichana na wanawake kujifungua kisha kuwatupa watoto wao inaonekana kuendelea kuwa sugu katika maeneo mbalimbali nchini.Mtoto Thomas anahitaji msaada kwa kuwa hafahamiki hadi sasa mama yake wala baba yake, kama umeguswa na unapenda kumsaidia mtoto huyu mahitaji muhimu kwa watoto unaweza kutembelea wadi ya wazazi katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma ama wasiliana nami kwa baruapepe albano.midelo@gmail.com,au piga simu 0784765917.
Chanzo;Kwanza jamii

0 comments:
Post a Comment