Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WADAU wa elimu wamekubali kutumia teknolojia ya habari na
mwasiliano kufundisha na kujifunza ili kukabili tatizo la uhaba wa
walimu na vitabu linalokwaza maendeleo ya elimu nchini.
Hayo ni baadhi ya maazimio yaliyotokana na mjadala wa siku mbili
wakati wa kongamano la elimu ulioandaliwa na Taasisi ya Learning InSync
International kwa kushirikiana na British Council na kufanyika mjini
Moshi, Kilimanjaro.
Akizungumza kwenye kongamano hilo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Jenister Mhagama, alisema ili kuharakisha matumizi ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) shuleni, serikali
itaongeza kasi ya kuwaelimisha walimu na wanafunzi kuhusu matumizi ya
teknolojia itakayorahisishwa na kusambazwa kwa
mkongo wa taifa.
mkongo wa taifa.
“Pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia duniani, Tehama
pia itatuwezesha kuhimili tatizo la uhaba wa walimu na vitabu nchini,”
alisema Mhagama na kuongeza kwamba mwalimu atatumia kitabu kufundisha
wanafunzi wengi kwa wakati mmoja.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment