Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said thabit Mwambungu amelitaka jeshi la Polisi
Mkoani Ruvuma kufuata Maadili na kuheshimu Kanuni, Taratibu na Sheria za Nchi
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ameyasema hayo wakati Jeshi
la Polisi lilipofanya Maadhimisho ya kuukaribisha mwaka 2014 Sherehe
zilizofanyika katika Uwanja wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) sherehe
zilizotanguliwa na paredi la Kikosi cha kutuliza ghasia.
Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma amesema Kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kulinda mali za raia pamoja
na kutii mamlaka yaliyopo katika Dola kinyume na hapo nikulidhalilisha jeshi la
Police kimaadili.
Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema sifa ambayo inaliondolea heshima Jeshi
la Police heshima ni kuwa na moyo wa ubinafsi, chuki na visasi
visivyo na tija.
Naye Kamanda
wa polisi anayehamia Manyara Deusdedit Nsmeki amesema katika kuukaribisha mwaka
2014 Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma linajivunia kwa asilimia 75% kupunguza
ujanji na kuweza kukamata nyara za serekari pia kuwa karibu na wananchi
Kamanda wa Polisi Deusdedit Nsmeki amesema jambo
lingine la kujivunia ni kupungua kwa ajali za barabarani kutoka maelfu ya ajali
kwa kila mwaka na kubaki katika mamia ya ajali. Jeshi la Polisi litaendelea
kutoa Elimu ili kupunguza ajali.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment