Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MTUHUMIWA wa mauaji ya
kulipiza kisasi cha kukataliwa kimapenzi, Bonas Mripa (38), amefikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Tunduru kujibu tuhuma
za mauaji ya watoto wawili.
Akiwasomea shtaka hilo
la mauaji namba 5/2014 mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Felix Nyalada,
Mwendesha Mashtaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Inspekta Songelael Jwagu,
alidai kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kosa hilo Agosti7, mwaka huu kwa
kuwaua watoto wawili Vairetih Nilai (8) na mdogo wake Cosmas Nilai (5).
Inspekta Jwagu alidai
kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kula njama na kuua watoto hao baada ya
kuvamia nyumba walimokuwa wakiishi na kuichoma moto wakati walipokuwa
wamelala saa 7 usiku.
Inspekta Jwagu alidai
kwamba, kosa hilo ni kinyume cha kifungu namba 196 sura ya 16 cha kanuni
ya adhabu kama ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 2002.
Hata hivyo, mtuhumiwa
huyo hakutakiwa kujibu shtaka hilo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka
ya kusikiliza kesi hiyo. Kwa mujibu wa Inspekta Jwagu, upelelezi wa
shauri hilo bado haujakamilika na mtuhumiwa alirejeshwa rumande hadi
Agosti 22, mwaka huu kesi inakapotajwa tena.
Taarifa za awali
kuhusiana na tukio hilo zinaeleza kuwa, chanzo cha mauaji hayo ni
kulipiza kisasi baada ya mtuhumiwa kukataliwa kimapenzi na mama wa
watoto hao
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment