Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Polisi Mkoa wa Ruvuma imeingia matatani baada ya askari wake
kudaiwa kumpiga risasi dereva wa bodaboda, Sallgo Nduguru (22) na
kumjeruhi kiganja na paja la mguu wa kushoto.
Inadaiwa kuwa, dereva huyo alifikwa na mkasa huo
baada ya kutaka kumpora silaha mmoja wa askari waliomkamata kwa kosa la
usalama barabarani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Mihayo
Msikhela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi
walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia zilizotokea
baada ya madereva wengine wa bodaboda kutaka kupambana na askari.
Kamanda Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea
saa 12 jioni katika eneo la Kombezi, Mfaranyaki, Manispaa ya Songea na
kudumu kwa muda wa dakika 30.
Kwa mujibu wa Kamanda Msihkela, askari polisi
wawili waliokuwa doria walimkamata kijana aliyetambulika kwa jina moja
la Aggrey kwa kosa la kuvunja sheria za usalama barabarani, lakini
dereva huyo alimpigia simu mmiliki wake, Sallgo Nduguru ambaye naye ni
dereva wa bodaboda na kuja na kundi la madereva wengine.
“Baada ya mmiliki huyo kufika na madereva wengine
walianzisha vurugu, ambapo Nduguru alidaiwa kutaka kumpora mmoja wa
askari hao silaha,” alisema.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment