WATAALAMU KUTOKA WIZARA YA NISHATI NA MADINI WAENDELEA KUWAPIGA MSASA WACHIMBAJI WADOGO JUU YA UCHIMBAJI BORA WA MADINI HUKO TUNDURU, RUVUMA

Kamishna Msaidizi- Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo, Mhandisi Fredy Mahobe kutoka Wizara ya Nishati na Madini akifafanua taratibu za kupata mikopo kwa wachimbaji wadogo. Mhandisi Heri Issa kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) akionesha jinsi uchekechaji wa madini unavyofanyika, katika mafunzo ya wachimbaji wadogo yanayoendelea huko Tunduru mkoani Ruvuma. Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Julius Sarota akielezea matumizi ya zebaki kwenye uchenjuaji wa madini katika mafunzo ya wachimbaji wadogo yanayoendelea huko Tunduru mkoani Ruvuma. Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini ( waliokaa...

PSPF YAZINDUA MPANGO MPYA WA UUZAJI NYUMBA KWA BEI NAFUU, SOMA HAPA KUJUA BEI ZAKE

Mfuko wa Pensheni wa PSPF unapenda kuutaarifu Umma kuwa umezindua Mpango Mpya wa uuzaji nyumba zake zilizojengwa kwa ajili ya makazi katika mikoa ya Dar es Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang’amba), Shinyanga (Ibadakuli) na Iringa (Mawelewele). Bei za nyumba ni kati ya sh. 52,000,000.00 hadi sh. 71,000,000.00 (bila VAT). Bei hizi ni kulingana na ukubwa wa nyumba na mkoa nyumba ilipo.   Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili hadi vinne. Chini ya utaratibu huu mpya unaoanza kutumika kuanzia Februari 2014; Muombaji atapaswa kuainisha kwenye fomu ya maombi aina ya nyumba anayohitaji na...

Wachimbaji wadogo watakiwa kuzingatia kanuni za usalama migodini

Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mhandisi Dkt. Crispin Kinabo akiwasilisha mada juu ya utunzaji wa mazingira kwenye migodi wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika mapema leo katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Mafunzo hayo yalishirikisha viongozi na watendaji wa wilaya, madiwani, wakuu wa vitongoji na wachimbaji wadogo lengo lake likiwa ni kuwapa uelewa wa kanuni za uchimbaji bora wa madini. Mmoja wa wakilishi wa wachimbaji wadogo ambaye ni mmiliki wa mgodi katika eneo la Mhesi Mapinduzi lililopo wilayani Tunduru Bi Sofia Hamdan akichangia mada wakati wa mafunzo hayo. Mpepo Ismail ambaye ni mmoja wa wachimbaji...

PSPF YATOA PONGEZI KWA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WA WIZARA YA FEDHA

MFUKO WA PENSHENI WA (PSPF)                         SALAMU ZA PONGEZI Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (MB)  Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mh. Adam K. Malima.  Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wanatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Saada Mkuya Salum (MB) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha. Vile vile, PSPF inatoa pongezi kwa kuteuliwa kwao Naibu Mawaziri wapya wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba (MB) na Mh. Adam K. Malima. Bodi ya Wadhamini...

Tunduru yapitisha bajeti YA MAENDELEO

HALMASHAURI ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imepitisha bajeti ya zaidi sh.bilioni 40.3 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kawaida ikiwa ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka 2014/15. Akisoma taarifa ya mapendekezo ya mpango wa bajeti ya halmashauri hiyo,Ofisa Mipango wa halmashauri hiyo, Kenneth Haule, alisema halmashauri hiyo inatarajia kukusanya zaidi ya sh.milioni 134.7 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida mishahara na mengineyo sh.bilioni 25.3. Alisema, bajeti hiyo imeongezeka kwa sh. bilioni 4.5 ambapo wanatarajia zaidi kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuweza kuongeza mapato ya halmashauri hiyo. Akichangia wakati wa kikao hicho Mbunge wa Jimbo la Kusini, Abdallah Mtutura, aliwataka...

MIKAKATI YA TENESCO KUHUSU UMEME MKOANI RUVUMA

 Engineer Boniface Njombe akitoa Elimu kwa Wandishi wahabari jinsi Umeme unavyo fanya Kazi akiwa na wafanyakazi wa Tenesco  Engineer Boniface Njombe akionyesha mashine zilizoko Katika Mtimbo iliyoko Kiblangoma Manspaa ya Songea  Engineer Boniface Njombe akicheza na Watoto eneo la Magagula Songea vijijini  Alipo ulizwa jinsi gani anajisikia kucheza na watoto Engineer alijibu kuwa hujisikia vizuri kucheza na watoto kwa kuwa hata yeye alipata malezi mazuri kutoka kwa watu tofautofauti jambo lililo mpa ujasiri alio nao hadi leo  Changamoto zipo pale unapo taka kitu kizuri hata Asali ni Tamu lakini utengenezaji...

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) UNAWATAKIA WATU WOTE SIKUKUU NJEMA MAULID

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF MAADHIMISHO YA SIKU YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Waisalamu na Watanzania wote katika kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) “PSPF TULIZO LA WASTAAFU” Mkurugenzi Mkuu, PS...

SALAM ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ali Mohamed Sheni pamoja na wananchi wote wa Tanzania katika kuadhimisha miaka hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar, 12 Januari 2014.    Kwa Mahitaji yako ya Hifadhi ya Jamii PSPF ni chaguo lako, Jiunge sasa “PSPF TULIZO LA WASTAAFU” Mkurugenzi Mkuu, PS...

SALAM ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ali Mohamed Sheni pamoja na wananchi wote wa Tanzania katika kuadhimisha miaka hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar, 12 Januari 2014.    Kwa Mahitaji yako ya Hifadhi ya Jamii PSPF ni chaguo lako, Jiunge sasa “PSPF TULIZO LA WASTAAFU” Mkurugenzi Mkuu, PS...

TATIZO LA UKOSEFU WA UMEME RUVUMA KUMALIZIKA MWAKA 2015

Mkoa wa Ruvuma unatarajia kuondokana na tatizo la umeme ifikapo mwaka 2015 baada ya mradi wa umeme kutoka Luli Chipole kukamilika na kuweza kutoa MG 8 ambazo zitasaidia kusambazwa katika Wilaya ya Mbinga, Nyasa na Songea. Naibu Mkurugenzi wa TANESCO Bonifance Njombe ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari kuelezea kero ya umeme inayoukabili Mkoa wa Ruvuma. Naibu Mkurugenzi amesema mahitaji halisi ya umeme kwa Mkoa wa Ruvuma ni MG 4.3 lakini kwa sasa umeme unaopatikana ni MG 1.6. Jambo linalosababisha kuwepo kwa mgao. Amesema hayo yote yanatokana na kuharibika kwa Mashine 3 zinazosambaza umeme katika Manispaa ya Songea. Naibu Mkurugenzi wa TANESCO Bonifance Njombe amesema kutokana na jitihada za Shirika la umeme Mashine mbili zimeshatengenezwa na kuweza kupunguza...

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) WAOMBOLEZA MSIBA WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DKT. WILLIAM A. MGIMWA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Wizara ya Fedha na Familia ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William A. Mgimwa Mfuko utamkumbuka kwa ushauri wake na ushirikiano aliouonyesha akiwa Waziri wa Fedha katika kufanikisha maendeleo na ustawi wa Mfuko. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMIN...

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) WAOMBOLEZA MSIBA WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DKT. WILLIAM A. MGIMWA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Wizara ya Fedha na Familia ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William A. Mgimwa Mfuko utamkumbuka kwa ushauri wake na ushirikiano aliouonyesha akiwa Waziri wa Fedha katika kufanikisha maendeleo na ustawi wa Mfuko. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMIN...

WAZIRICHIZA AMSIMAMISHA KAZI KIGOGO

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Cristopher Chiza   Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Cristopher Chiza, amemsimamisha kazi mrajisi wa mkoa wa Ruvuma, Watsoni Nguniwa, kwa kushindwa kutatua kero zinazowakabili wakulima wa mkoa huo. Akitoa agizo hilo jjijini Dar es salaam Waziri Chiza alisema wakati umefika kwa watendaji wote wa wizara yake ambao watashindwa kwenda na kasi ya sheria mpya ya mwaka 2013 wapishe wenyewe kabla rungu la sheria hiyo halijawaangukia. Mrajisi huyo anatuhumiwa kushindwa kufanya ukaguzi kwa miaka minane na kushindwa kutatua matatizo ya wakulima ya wilaya nne za mkoa wa...

MLEMAVU WA KUSEMA NA KUSIKIA AMUUA BABA YAKE MZAZI KWA KUMTANDIKA NA MPINI WA SHOKA.‏

Kijana wa umri wa Miaka 29 mwenye ulemavu wa kushindwa kuongea (Bubu) aliyefahamika kwa jina la Zuberi Hatima Said anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Baba yake Mzazi  akiwa anamtuhumu kumroga. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki amemtaja Marehemu huyo kuwa ni Hatima Said Lung’ande (70) na kwamba katika tukio hilo mtuhumiwa alimuua kwa kumpiga na mpini wa Shoka. Kamanda Nsimeki aliendelea kufafanua kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 29 /2013 majira ya Saa 12  Jioni katika kitongoji cha Mchangani kilichopo katika Kijiji cha Kazamoyo Tarafa ya Lukumbule Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma. Alisema kuwa kufuatia hali hiyo mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani ili sharia iweze kufuata mkondo wake baada ya kukamilika kwa taratibu za mahojiano...

Serikali yaombwa kushirikiana na kampuni binafsi upimaji viwanja

 Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeombwa kuona umuhimu wa kuchukuwa makampuni binafsi ya upimaji wa viwanja ili kuwarahisishia wananchi upatikanaji rahisi wa viwanja badala ya kutegemea halmashauri ifanye kazi hiyo peke yake, anaripoti Cresensia Kapinga, Songea. Ombi hilo limetolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Namanyigu uliopo katika halmashauri ya Manispaa ya Songea Bw.Fidolin Malindisa wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi ya afisa mtendaji wa mtaa huo. Malindisa alisema kuwa mpango wa mzuri wa serikali wa kupima viwanja kupitia makampuni binafsi umeonekana kuwa na matunda mazuri kwa wakazi wa manispaa ya Songea baada ya mtaa wake kuibua...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa