Home »
» Tunduru yapitisha bajeti YA MAENDELEO
Tunduru yapitisha bajeti YA MAENDELEO
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imepitisha bajeti ya zaidi
sh.bilioni 40.3 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kawaida ikiwa ni
pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka 2014/15.
Akisoma taarifa ya mapendekezo ya mpango wa bajeti ya halmashauri hiyo,Ofisa
Mipango
wa halmashauri hiyo, Kenneth Haule, alisema halmashauri hiyo inatarajia
kukusanya zaidi ya sh.milioni 134.7 kutoka katika vyanzo vyake vya
mapato kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida mishahara
na mengineyo sh.bilioni 25.3.
Alisema, bajeti hiyo imeongezeka kwa
sh. bilioni 4.5 ambapo wanatarajia zaidi kuimarisha ukusanyaji wa mapato
ya ndani ili kuweza kuongeza mapato ya halmashauri hiyo.
Akichangia
wakati wa kikao hicho Mbunge wa Jimbo la Kusini, Abdallah Mtutura,
aliwataka madiwani kusimamia mapato kwani wao ndiyo wanaojua namna
mapato yanavyovuja kwani wao ndiyo wanaoishi na wakusanya ushuru.
Aliwataka madiwani hao wasimamie pia matumizi ya fedha walizokusanya
ikiwa ni pamoja na kuacha kufanya siri bali wawafichue wanaohujumu
mapato ya halmashauri hiyo
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment