Kijana
wa umri wa Miaka 29 mwenye ulemavu wa kushindwa kuongea (Bubu)
aliyefahamika kwa jina la Zuberi Hatima Said anashikiliwa na Polisi kwa
tuhuma za kumuua Baba yake Mzazi akiwa anamtuhumu kumroga.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki amemtaja Marehemu huyo
kuwa ni Hatima Said Lung’ande (70) na kwamba katika tukio hilo mtuhumiwa
alimuua kwa kumpiga na mpini wa Shoka.
Kamanda
Nsimeki aliendelea kufafanua kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 29 /2013
majira ya Saa 12 Jioni katika kitongoji cha Mchangani kilichopo katika
Kijiji cha Kazamoyo Tarafa ya Lukumbule Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma.
Alisema
kuwa kufuatia hali hiyo mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani ili
sharia iweze kufuata mkondo wake baada ya kukamilika kwa taratibu za
mahojiano yatakayo washirikisha wataalamu wa Lugha za alama.
Akizungumzia
tukio hilo mkalimani wa familia hiyo Mtoto wa kwanza kati ya watoto
wane wa marehemu Lung’ande Bw.Adamu Sadiki alisema kuwa kabla ya tukio
hilo ndugu yake huyo ambaye ni kati ya watoto watatu wa marehemu wenye
ulemavu huo alidaikuwa kwa muda mrefu amekuwa akimuona marehemu usiku
akiwa anamuwangia.
“Tumezaliwa
watoto Wanne katika familia yetu kwa Baba na mama Lung’ande lakini
kutokana na mipango ya mungu wenzangu wote ni mabubu hivyo mimi nimekuwa
kiunganishi kikubwa katika familia, wageni pamoja na ndugu na jama”
alisema Bw. Adamu na kuongeza kuwa Zuberi amekuwa akimlalamika baba kuwa
ni mchawi siku za hivi kalibuni hali ambayo iliwaweka katika mazingira
ya utata miongoni mwao.
Mganga
aliye ufanyia uchunguzi mwili wa Marehemu Lung’ande, Dkt. Joseph
Ng’ombo alisema kuwa kifo hicho kilisababishwa na tukio la kutokwa na
damu nyingi kufuatia kipigo hicho. Alisema katika tukio hilo marehemu
aliumia vibaya Kichwani upande wa jicho la kulia pamoja na kupasuka kwa
fuvu la kichwa chake na jicho la Kulia kufutia kipigo hicho.
0 comments:
Post a Comment