Home » » WAZIRICHIZA AMSIMAMISHA KAZI KIGOGO

WAZIRICHIZA AMSIMAMISHA KAZI KIGOGO

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Cristopher Chiza
 
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Cristopher Chiza, amemsimamisha kazi mrajisi wa mkoa wa Ruvuma, Watsoni Nguniwa, kwa kushindwa kutatua kero zinazowakabili wakulima wa mkoa huo.
Akitoa agizo hilo jjijini Dar es salaam Waziri Chiza alisema wakati umefika kwa watendaji wote wa wizara yake ambao watashindwa kwenda na kasi ya sheria mpya ya mwaka 2013 wapishe wenyewe kabla rungu la sheria hiyo halijawaangukia.

Mrajisi huyo anatuhumiwa kushindwa kufanya ukaguzi kwa miaka minane na kushindwa kutatua matatizo ya wakulima ya wilaya nne za mkoa wa Ruvuma za Namtumbo, Tandahimba, Songe na Mbinga.

“Sheria ya sasa haitaki mchezo, sasa kama kwa pamoja tumeamua kusimamia kero zinazowakabili wakulima halafu mwingine anakwamisha, ni lazima awajibishwe,” alisema Waziri Chiza katika mahojiano na NIPASHE.

Waziri Chiza alisema baada ya sheria mpya kuanza kufanyakazi anawataka maafisa kilimo wote nchini kuhahikisha wanatatua matatizo ya wakulima bila kushurutisha.

Hata hivyo, alisema kumekuwa na uwelewa mdogo kuhusu wizara yake na kwamba wananchi wamekuwa wa nalalamika kuhusu masoko ya bidhaa za kilimo. 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa