Mkoa wa Ruvuma unatarajia
kuondokana na tatizo la umeme ifikapo mwaka 2015 baada ya mradi wa umeme kutoka
Luli Chipole kukamilika na kuweza kutoa MG 8 ambazo zitasaidia kusambazwa
katika Wilaya ya Mbinga, Nyasa na Songea.
Naibu Mkurugenzi wa TANESCO
Bonifance Njombe ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari
kuelezea kero ya umeme inayoukabili Mkoa wa Ruvuma.
Naibu Mkurugenzi amesema
mahitaji halisi ya umeme kwa Mkoa wa Ruvuma ni MG 4.3 lakini kwa sasa umeme
unaopatikana ni MG 1.6. Jambo linalosababisha kuwepo kwa mgao. Amesema hayo
yote yanatokana na kuharibika kwa Mashine 3 zinazosambaza umeme katika Manispaa
ya Songea.
Naibu Mkurugenzi wa TANESCO
Bonifance Njombe amesema kutokana na jitihada za Shirika la umeme Mashine mbili
zimeshatengenezwa na kuweza kupunguza kero za mgao wa umeme, Mashine ya mwisho
ikishapona itasaidia kuwa na umeme wa ziada KW 400.
Naibu Mkurugenzi wa TANESCO
amesema mashine zinazotumia maji za chipole zikikamilika zitaweza kutoa MG Wat
8 wakati Matumizi ya Chipole ni MG 1 moja tu jambo litakalouwezesha Mkoa wa
Ruvuma kuwa na Migawat 14 ambazo zitasambazwa wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma.
0 comments:
Post a Comment