Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa amewaonya baadhi ya
wanachama wanaochafuana na waliojitokeza kutangaza nia ya kugombea
nafasi mbalimbali za udiwani, ubunge kabla ya wakati akiwamo mwenyekiti
wa chama hicho mkoani hapa, Joseph Fuime.
Mwenyekiti huyo anadaiwa kutangaza nia ya kugombea
ubunge wa Jimbo la Songea mjini na kutakiwa kuacha mara moja, kabla ya
hatua kali za kinidhamu hazijachukuliwa dhidi yao kama kanuni ya chama
hicho inavyosema,ikiwamo pamoja na kufukuzwa uanachama, kusimamishwa au
kupewa adhabu zilizopo kwenye kanuni.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana
kuhusu onyo lake Dk Slaa amesema, kutangaza nia siyo dhambi ni haki ya
mwanachama na siyo mgogoro ila anapaswa afuatae kanuni za chama
zinavyoelekeza na iwapo kanuni zitavunjwa na mgombea basi hawatasita
kumchukulia hatua.
“Ni kweli kuna baa dhi ya wanachama wanatangaza
nia na hawafuati kanuni zinavyosema,tayari chama kimeshapeleka waraka
katika majimbo, wilaya na mkoa wasome na kuelewa,iwapo hawajapata waraka
huo wawasiliane na ofisi yangu watumiwe kwani wakibainika watapata
matizo pamoja na kuchukuliwa hatua za kinidhamu,”alisema Dk Slaa.
Mwenyekiti wa chama hicho Singida, Joseph Fuime
hakuweza kupatikana kuzungumzia tuhuma hizo kwani simu zake zote za
mkononi hazikupatikana.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment