Home » » Diwani apinga ongezeko la mitaa, kata

Diwani apinga ongezeko la mitaa, kata

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
DIWANI wa Misufini katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Ruvuma, Salum Mfamaji (CHADEMA), amesema kuongezwa kwa mitaa katika manispaa hiyo ni kuibebesha mzigo serikali na wananchi.
Mfamaji alisema hayo wakati akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani humo kilichofanyika chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Charles Mhagama.
Alisema mantiki ya kuendelea kuongeza mitaa wakati iliyopo kuihudumia kwake ni matatizo huku akisisitiza kwamba kuendelea kuongeza kata wakati watendaji wa mitaa na kata wanalipwa mishahara midogo isiyokidhi mahitaji yao kwa mwezi badala yake iwaboreshee mishahara yao.
 Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa