Home » » Mamba amuua mvuvi Mto Lwika

Mamba amuua mvuvi Mto Lwika

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MASALIA ya mwili wa Charles Mkoma (37), mwanakijiji wa Liuli, wilayani Nyasa, Ruvuma yamekutwa kandokando ya Mto Lwika.
Mkoma, aliuawa baada ya kukamatwa na mamba wakati alipokwenda kuvua samaki kwenye mto huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Akili Mpwapwa, alisema mabaki hayo yalipatikana mchana wa Machi 8, mwaka huu.
Akifafanua zaidi alisema mabaki ya mwili wa marehemu huyo yaligunduliwa na watu waliokuwa wakimtafuta baada ya kutooneka nyumbani kwake kwa siku nne.
 Chanzo;Tanzaniz Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa