Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wananchi
wa vijiji vya Mtyangimbole na Gumbiro Songea Vijijini baada ya miezi
miwili wanatarajia kuvuna kilo 500 za Asali na Nta kilo
50 baada ya kutundika mizinga 50 katika Msitu wa Hifhadhi
Mkuu
wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Said Thabiti Mwambungu amesema hayo katika wiki ya kitaifa ya kutundika
mizinga iliyo fanyika kijiji cha Mtyangimbore .Amesema Mpango wa serekari wa
Matokeo Makubwa sasa ni kubuni mipango mbali mbali ya kumwongezea Mwananchi wa
Chini kipato kupitia Ufugaji wa Nyuki’
Mkuu
wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti amesema umefika wakati sasa wa
kujenga urafiki na Nyuki badala ya kuwaona Nyuki kama Adui amewataka wananchi
kuepuka na kuchoma misitu ovyo unao sababisha viumbe wengi kutoweka
wakiwemo nyuki.
Mkuu wa wilaya ya Songea
Joseph joseph Mkirikiti akimwakilisha mkuu wa Mkoa Said thabit Mwambungu
amesema Serekari ina buni mbinu mbali mbali kuongeza kipato kwa Mwananchi
kupitia Mali asili tulizo nazo nyuki walioko wapatao milioni 9.2 wakitunzwa
vizuri wataweza kuongeza hali ya uchumi kukua ikiwa pamoja na kuongeza fedha za
kigeni ,Hivyo tabia ya kuangamiza viumbe vyenye kuleta tija iachwe mara moja
Meneja wa Misitu Wilaya ya
Songea Manyisye Mpokigwa amesema juhudi za Idara yake kuhusu Utundikaji wa
Mizinga na kulinda Misitu sasa inaonyesha mafanikio wananchi wengi wa vijijini
wameanza kuvuna Asali .
Naye Mwakilishi wa Meneja wa
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Gaudens Kilasi amesema kutokana na Mizinga
25 iliyotolewa mwaka jana na mizinga 25 ya sasa itawasaidia wananchi kuvuna
Tani 500 za Asali swala litakalo saidia kupunguza umasini kwa wananchi wa
vijijini.
Mkuu wa Wilaya ya Songea
Joseph joseph Mkirikiti amesema Jumla ya Makundi Milioni 9.2 ya nyuki yapo
hatarini kutoweka endapo wananchi hawataacha mtindo wa kuchoma Misitu ovyo,
amewaomba Wananchi kuacha kuwa Maadui na Nyuki au Misitu sasa wawe marafiki kwa
Nyuki.
0 comments:
Post a Comment