Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wananchi wa Mkoa wa
Ruvuma wameisifu SUMATRA kwa kuweza kusimamia safari za Mabasi na kufanikisha
kupanga safari katika sehemu ambazo zilikuwa ni kero kwa Wananchi wa Mkoa wa
Ruvuma.
Mohamed Chichi akizungumza kwa niaba ya Wasafiri katika Kituo
Kikuu cha Mabasi Songea, amesema katika Changamoto zilizokuwa zinawakabili
Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ni kukosa Usafiri wa Songea – Dodoma, Songea –
Mwanza na Songea – Mbamba Bay. Njia zote hizo zimefunguka tunaishukuru Serikali
kwa kuweza kutatua changamoto hizo.
Afisa Mfawidhi wa
SUMATRA Mkoa wa Ruvuma Denis Daudi amesema Mkoa wa Ruvuma una changamoto nyingi za
usafiri, Ukiwemo usafiri wa Songea – Mkenda –njia inayo unganisha na Nchi ya Msumbiji na Tanzania ,na Songea Tunduru bado kunahitajika Usafiri wa
uhakika,
Barabara ya Songea –
Mkenda serekali ina fanya mipango ya kumpata mfadhili ili atengeneze njia hiyo kwa kiwango cha Lami itaweza kufungua
mawasiliano kati ya Msumbiji na Tanzania. Amewataka wananchi kuwa watulivu wakati juhudi za
serekali zikitafuta njia ya kutatua changamoto hizo
0 comments:
Post a Comment