Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZABUNI wa vyakula katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea,
wameikumbusha serikali kuangalia uwezekano wa kuwalipa deni lao la
zaidi ya sh bilioni moja lililotokana na kulisha katika shule za
sekondari, vyuo na taasisi mbalimbali mkoani hapa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima jana,
wazabuni hao ambao hawakutaka kutajwa majina, walisema pamoja na ahadi
nyingi za viongozi wa kitaifa kutolewa juu ya kulipa madeni hayo,
lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.
Walisema mbali ya Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Mhagama, kuwaahidi
waendelee na kazi ya kulisha katika shule na vyuo wakati malipo yao
yakishughulikiwa, jambo hilo hadi sasa limekuwa hadithi.
Walisema wamekuwa wakiendesha shughuli ya kulisha kutokana na mikopo
inayotolewa kwenye taasisi za fedha, jambo ambalo wamedai hivi sasa
limewaweka mahali pabaya kutokana na taasisi hizo kutaka kuuza mali zao
kutokana na kuchelewesha marejesho.
Walisema endapo serikali haitaharakisha malipo hayo, watashindwa
kuendelea kulisha katika shule hizo, kwani fedha iliyotumwa kwenye
baadhi ya shule za sekondari na vyuo kiasi cha sh milioni 72 hazitoshi
kwa kugawana wazabuni wote kwani zinatosha kulisha kwa siku 40 tu.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment