Jana akiahirisha bunge, makamu mwenyekiti aliwakumbusha wajumbe kuwa wasome karatasi walizogawiwa kwa kuwa leo watafanya maamuzi magumu ya kubadili kanuni, ni kanuni zile zinazopigiwa upawa na ukawa, huenda kanuni ya theluthi mbili ili wapitishe katiba yao kilaini.
---------------------
Manda
Anawasilisha azimio la kufanya marekebisho ya kanuni kutoka na vifungu vya 56 na 57 ya kanuni za bunge maalum.
-kanuni ya 32,33,35,41,60, 62 na kanuni ya 82.
-yatasomwa iwe yatawasilishwa.
-Msingi wa kufanya marekebisho ni kuweka utaratibu mzuri kwa wajumbe kupeleka majedwali katika kamati zao badala ya kwenye bunge
. inapendekezwa kufutwa kwa utalratibu wa awali wa kuleta mapendekezo bungeni.
. kurekebisha ili maoni ya wachache wasome wenyewe.
Suzan Marwa anasema;
tumekuja kutunga katiba ya wananchi sio ya chama. Kitu ambacho kinafanya watu tushindwe kuelewana ni muundo wa serikali. Hii ndo imefanya watu hadi watoe maneno machafu.
Haya maneno ya wananchi watu wanasema sio sahihi. Mi napendekeza turudi kwa wananchi tuwahoji wananchi tena kwa hivi vifungu kama wanataka serikali mbili au tatu. Haya tunayo yafanya sio wananchi wanayotegemea.
Miaka 50 ya uhuru wananchi wanalala chini hawana madawa wala huduma. Wananchi wanataka katiba itakayo watua mzigo huu.
Miaka hamsini ijayo inaweza kuwa si mizuri sababu ya uchu wa madaraka.
Mimi siwezi kuikashifu rasimu ya walioba kwa sababu tumeweza kujua kero za wananchi ambapo tunaweza kukaa chini na kufanyia marekebisho tukapata katiba njema. Hasira hukaa kifuani kwa wapumbavu. Kitu kizuri kule na ndugu yako, ndugu yako ni wananchi walio njee. Leo tupo katika uongozi kesho hatupo kwenye uongozi watoto wetu watarothi nini?
Nawasihi wajumbe tutumie malidhiano ndipo tutafika mwisho. Haya marumbano tunayo yafanya hayawasaidii wananchi.
Isack Cheyo anasema:
Tujielekeze katika kutunga Katiba sio kejeli na maneno. Wangetuletea katiba yenye serikali moja, mbili, tatu ili tuchague tofauti na hizi walosema serikali tatu tu.
Sijafurahia wanao mkejeli Mh. Warioba. Inanisikitisha sana sababu tangu tuanze kujadili muundo watu wamekua wakijiita wazanzibar baadala ya watanzania na hii ni kwasababu hiki kitu kinachoitwa Tanzania Zanzibar. Watu wa visiwani wapo makini sana na haya mambo sabau ya udogo wao na uchache wao. Utasikia sisi wazanzibar tunataka nini tena? tumepewa oic, bendera.' Haya mambo sio mazuri. Tungeanza na utanzania kwanza kuliko huu uzanzibar kama mwl. alivo iacha. Mwalimu aliacha taifa moja yenye serikali mbili. lakini leo hii tuna serikali mbili na mataifa mawili.
Nakubaliana na kiswahili iwe lugha ya taifa lakini tusibeze kingeleza ambayo ni kiswahili cha ulimwengu. Haya matusi ya kiswahili tunayosema humu tunawafunza wanetu. Sikukuu ya 12 dec ni sikukuu ya Tanganyika. tukubali hiyo kuna kosa gani kuitaja tanganyika?
Siku moja Tanganyika itakuwepo na Itakuwepo kwa hadhi yake ile ile. Asanteni sana
Usi Sumali anasema;
watu wanazungumza swala la zanzibar wamekiuka katiba na uwezo wa rais wa zanzibar.
Baraza la mitihani kuna tatizo la uwazi.
Mfuko wa elimu ya juu nawapongeza. lakini tatizo lililopo ni la uwiano katika scholarship, kulipa kodi mara mbili, haya matatizo yaangaliwe.
Swala la rais wa zanzibar kuondolewa kwenye makamu wa rais wa Tanzania. Kwenye ajira uwiano sio mzuri hivi viangaliwe upua
Yusuph Omar Chunda anasema;
Swala la Muungano huu tusiuchezee kwani una historia kubwa. Mimi mnina asili ya bara lakini nimezaliwa zanzibar na baba yangu amezaliwa zanzibar. siwezi kukuelewa ukiniambia muungano uteteleke.
Tumshukuru Nyerere na Karume waliotuunganisha. Watu 14 walioleta mapinduzi tuwashukuru pia, ndg said abdallah natepe, hamis duruheshi mhamed kauole hamisi ndui abdala mfalanyaki washoto mokero pili sulemani amir haji, saidi seif bakari omar ndo waliosababisha kuikomboa zanzibar. Nazani hata kesho wanaweza kumbukwa pia.
Changamoto za muungano zipo na zinafaa zishughulikiwe. Rais wa zanzibar achukue nafasi yake.
Lugha ya kiswahili kimetusaidia kutuunganisha na kuleta amani zaidi.
Natoa ombi kwamba vyombov ya habari tbc na zcb Upande wa radio.
Anna Abdallah anasema:
Nlikua mwenyekiti wa kamati namba kumi. nlipewa mapendekezo
1. Tanzania si shirikisho ni jamhuri ya muungano wa Tanzania
2.Vyombo vya shirikisho tulipendekeza viwe vya Muungano.
Wenzetu hawana uvumilivu wa kusikia maneno ya wenzao. Hili ndio tatizo kubewa sana. sisi tulioko humu ndani ndio tunaotunga katiba ya Watanzania.
Mambo mengine lazima kuvumiliana. Kila mtu ana uhuru wa kuonge yaliyo yakwake. Lakini la kuwakashifu wasisi hilo halisameheki na halikubaliki. Kuwatukana wasisi ni sawa na kuwatukana wazazi wako. mtu wa hivyo inabidi apimwe akili.
Zamani hatukujua huyu ametoka zanzibar au bara hata huko wenzetuhawajui, wanajua sisi ni Watanzania. Mimi ni Muumini wa serikali mbili
Kingunge.
Nawashukuru sana waganga wa tiba asili kwa kunifanya nije hapa. Mimi nlikua mlezi wa chama hiki tangu 1998. Waliokua wanahoji walitaka watu waseme kwamba nimepenyapenya lakini mimi nimependekezwa na hiki chama. Ni chama cha heshima kwani kinatoa dawa za miti shamba sio ramli.
Haya mambo mliokua mnafanya ya kuzomea si sawasawa. kuna lugha zimetumika hazifanani na sisi wala Watanzania. Lugha za ugomvi na kudhalilisha.
Lugha za kudhalilisha wasisi wetu eti mwalimu Nyerere si Mungu je nani alikuambia ni Mungu?
Watu tumewasomesha . Swala kubwa la msomi ni unyenyekevu. Hapa tunapishana kwa mawazo tu. Hata rasimu hii ina mawazo tu, hakuna watu mle ndani ya rasimu. Hapa hatuwazungumzi wajumbe wa timu, Warioba bali tunazungumzia haya mawazo yaliyo katika rasimu. Tuache kumshambulia Walioba. Chama changu CCM kina adabu sasa wewe unamshambulia walioba unafedhehesha chama changu.
Mazungumzo tuliyo yafanya sura ya 1 na 6 tumefanya vizuri sababu maoni ya walio wengi na wachache yamejitokeza. Lakini kazi ya kufanya maamuzi bado.
Maoni yangu mimi; Sisi hapa tumetumwa na wananchi ili ipatikane katiba mpya iliyo bora sio ilimradi katiba.
Inabidi kwanza ijue katika miaka hii 50 tuna mafanikio makubwa kwa hiyo katiba bora lazima izingatie yale mazuli mfano Muungano wetu, Haya yote mafanikio yametokana na Muundo wa namna wake wa Serikali mbili.
Tunataka katiba itakayo punguza au kuondoa kero za Muungano, kama tutashindwa kuondoa hayo mapungufu itakua sio katiba bora. Naamini tutatumia kipindi hiki cha kupumzika kutafakari hili.
Tumeishi duniani na tumejifunza mambo. Katiba mpya lazima ilete mambo ya msingi na kuondoa hili kero la Umasikini uliokithili wa Nchi yetu. Mtaandika katiba lakini kama mtashindwa zungumzia Umasikini itakua sio katiba bora, Katiba mpya lazima izungumzie uchumi wa watanzania walio wengi.
Kupata katiba Mpya lazima kuwepo na maelewano humu ndani. Waliotoka nje walionyesha mapungufu makubwa lakini tunaomba warudi na wakirudi naomba tuelewane. Kupata theruthi mbili ya bara na zanzibar ni sheria.
Kule zanzibar kulilkuwepo na tatizo tangu mwaka 1998 limedumu kwa miaka 18 kila siku tunazungumza baadae tukaelewana tukazungumzi na Hamad rashid Nahodha mimi mwisho wa siku tukapata fomula maalim Seif sasa hivi ni Makamu Rais wa kwanza ni kutokana na Mazungumzo.
Sasa tunzungumze mpaka tuelewane na wakubwa nao inabidi wazungumze.Asante kwa kunivumilia may 30 ntafikisha miaka 82 si haba. asanteni sana
Kificho anasema:
Mimi nimeshangaa sana watu wanaosema eti mimi naunga mkono serikali tatu, Tangu lini?
Mimi nasema naunga mkono serikali mbili ambazo zimedumisha Huu muungano wetu kwa miaka 50.
Balozi Seif Idd (makamu wa pili wa rais zanzibar) anasema ;
Mimi naungana na walio wengi kwamba muungano wetu huu uwe wa walio serikali mbili. Wananchi wametuleta humu ili tuwapelekee katiba itakayokua kwa masirahi yao. Tumetumia gharama kubwa kutengeneza ukumbi huu ili tukae tustarehe lakini wenzetu wakaamua kutoka nje. Nawaomba warudi sababu katiba haitungwi Barabarani wala popote pale isipokua humu ndani tu.
Humu ndani kila mmoja nalipwa sh laki tatu kila siku tunayo kaa humu. kwa siku70 tulizopangiwa tumetumia bil 20 mpaka sasa. ndizo tulikua tutumie mpaka leo hii. pesa nyingi zimetumika katika kutunga kanuni baada ya hapo kujadili siri au wazi. watu wakang'ang'ana sana kura ya siri. Lakini wale wale waliotaka kura za siri wakapiga wazi. uharibifu wa fedha.
sura ya kwanza na ya sita tu ndo zimetumia bil 20. Leo tunaahilisha mpaka tarehe 5/8. Rais alikubali kuongeza siku 60 sasa tuangalie siku 60 tutatumia kiasi gani. Nia yetu humu ndani ya kutunga katiba. Watu wameshindwa kutunga katiba wameanza mwalimu nyerer karume na kombo wakati hawawezi kuwajibu.
Mimi naomba wenzetu warudi waje tujadili katiba mpya ambayo wananchi wametutuma. Kero hizi za Muungano zinaweza kutekelezeka kwa muundo huu wa Muungano tulionao.
Nawasihi wenzetu walio toka warudi. asanteni.
Peter Pinda anasema;
Mimi nilikua kamati namba moja. Nlikua nasikiliza mjadala huu kwa makini sana. tanzania ni miongoni mwa Nchi barani afarika ambayo tumeweza kuwa wamoja kutokana na muungano wetu ulio asisiwa na wasisi wetu. Mijadala iliyopita ilikua na vijembe na kejeli. Naishukuru kamati yako ya kanuni kwa kuendelea kuboresha kanuni hizi. Tunapokwenda tutajipanga vizuri zaidi.
Muungano wa Zanzibar na Tanganika umeelezwa na kuandikwa sana lakini ni vizuri tuendelee kuyaheshimu mawazo ya waasisi wetu wa Muungano.
Watu wanajaribu kulilia kitu ambacho hawajaexperience hata kidogo, nashangaa sana. Tanganyika imedumu mwaka mmoja na nusu lakini miaka 50 tupoTanzania. Tunaitaka Tanganyika Tanganyika ipi hyo?.
Mwalimu si mtu ambaye unaweza kumbeza kwa kiasi hicho kwani anaheshimika dunia nzima. Leo mtu anasimama kijana wa juzi anatumia lugha chafu kwa baba huyu! jamani.
Nikweli kero za muungano zipo. kweli muungano ulikua na kero 31 leo zimebaki 6. Ibara ya109 katika rasimu hii wameunda tume ya kushughulikia kero za Muungano. Nawashukuru sana tume ya Warioba kwa hili.
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Hawa wenzetu waliotoka nawaomba kwa dhati kabisa warudi. Katiba yoyote kazi kubwa inayofanyika ni ya ujenzi wa katiba. Tuliwambia tuboreshe hii wakakataa eti wanataka mpya, mpya kwani ndo tunapata uhuru? sasa kipi kipya kilichoingia kwenye hii?. Siafiki hata kidogo kwamba tume imetumia fedha nyingi kwa hiyo inabidi iletwe ya serikali tatu,
Watu wametazama takwimu wamehoji.
wakati wa kuwasilisha wrasimu ya katiba limerudia sana kwamba ofisi ya waziri mkuu imependekeza serikali tatu. Mimi sikua ndani yake bali mimi nlitoa maoni yangu kama mimi. Na hii ya kutumia ofisi hizi mbili kupendekeza serikali tatu kwamba wananchi ndo wamependekeza hivyo sio sahihi hata kidogo.
Nawashukuru tume kwa kufanya kazi nzuri. Asanteni sana.
Samwel Sitta anasema;
Maoni ya mapendekezo tuliyo yatoa sasa tunayakabidhi kwa katibu ili wapewe kamati ya waandishi. leo saa kumi jioni Rais atatoa Hotuba katika ukumbi wa TPA sabasaba kuhusu mambo ya Muungano.
Wajumbe wanahojiwa kama wanaafiki wote wamesema ndio.
-Kiti kimetuhumia hatukuweza kudhibiti matusi. kanuni hazikusema hivyo bali ni kuwaondoa nje ikibidi kwa nguvu. tulisita kwa kuwe kungetokea ugomvi.
-Nilifanya ziara kwa viongozi wa dini bado sijamaliza. ntatembelea makundi mbalimbali. Wale wenzetu ambao hawapo hapa labda tuliwakasirisha basi ntafanya jitihada kupitia vyama vya siasa ili tukirudi turudi nao.
Anasoma dua ya kushukuru na kumaliza.
Bunge limeahirishwa hadi tarehe 05 .08 . 2014 siku ya Jumanne saa tatu asubuhi.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Home »
» Dondoo za yanayojiri Bungeni Dodoma leo Ijumaa Trh 25 Aprili 2014
0 comments:
Post a Comment