Home » » Meja Jenerali Msemwa kuzikwa leo

Meja Jenerali Msemwa kuzikwa leo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399

MWILI  wa  aliyekuwa  Meja Jenerali  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),  Kevin Msemwa, umewasili  mjini Songea  na  kupokewa na viongozi mbalimbali wa  serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu.

Mwili  huo uliwasili  jana, saa 4 asubuhi kwa ndege ya jeshi   hilo  katika Uwanja wa Ndege wa  Ruhuwiko  wa mjini Songea na kuelekea  nyumbani kwa marehemu maeneo ya Seed Farm   mjini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwa  mwili huo, Luteni Jenerali na Mnadhimu wa Jeshi, Samweli Ndomba, alisema  marehemu Msemwa anatarajiwa kuzikwa leo saa 8 mchana katika makaburi ya  Mfaranyaki mjini Songea.

Msemaji wa familia, Nicas Msemwa, alisema kuwa Kevin  alifariki dunia Aprili 3, mwaka huu alipokuwa akipatiwa matibabu katika  Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam.

Nicas ambaye ni mdogo wa marehemu, alisema misa ya mazishi  itafanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba,  mjini Songea.

Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa