Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU
wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Chande Nalicho, amempongeza
Mwekezaji wa nyumba ya kulala wageni ya Peramiho, Faustin Chale kwa
uwekezaji alioufanya wilayani hapo.
Alisema ujasiri wa mwekezaji huyo wa kutumia mkopo wa sh milioni 100
kwa ajili ya mradi wa nyumba hiyo ni jambo jema alilodai kuwa
litapunguza adha ya malazi kwa wageni wakati wa sherehe za kimkoa na
ziara za viongozi wa kitaifa.
Nalicho alisema hayo jana alipozungumza na Tanzania Daima huku akiwataka wananchi wengine kuiga mfano wa mdau huyo wa maendeleo.
Alisema mwekezaji huyo mzawa ni mtumishi wa serikali hivyo anastahili
pongezi kwa aina hiyo ya uwekezaji wa gharama kwa ajili ya shughuli za
maendeleo huku wengine wakiogopa kukopa na kuwekeza wilayani humo kwa
madai ya miundombinu mibovu ya barabara.
Aliwataka watumishi wa serikali kutumia fursa ya kufunguka kwa
barabara kutoka Mtwara kupitia Tunduru na kutoka Tunduru hadi Songea
itakayojengwa kwa kiwango cha lami mapema mwaka huu kujiwekea vitega
uchumi vitakavyowasaidia baada ya kustaafu.
Kwa upande wake mmiliki wa nyumba hiyo, Faustin alisema asili ya
mafanikio na maendeleo yake ni kukopa hivyo amewashauri watumishi
wengine nao kuandaa maisha yao kwa kuweka vitega uchumi badala ya
kutegemea fedha za kiinua mgongo.
Mradi huo ulifunguliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Rachel
Kassanda wakati mwenge huyo ulipopita wilayani Tunduru mwishoni mwa
wiki.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment