Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru, Rachel Kassanda, amewataka
Watanzania kuacha tabia ya kuwahifadhi wahamiaji haramu, kwani kwa
kufanya hivyo ni kuhatarisha amani na usalama wa nchi.
Akizungumza baada ya kuzindua nyumba ya Ofisa Uhamiaji Mkoa wa
Ruvuma, Kassanda aliwalaumu wakazi wa maeneo mbalimbali ya mpakani
mkoani hapa kwa kuiweka rehani amani na usalama wa nchi bila sababu za
msingi.
Alisema uhamiaji pekee haiwezi kufanya kazi bila kushirikiana na
wananchi, hivyo wanapaswa kusaidia kwa kutoa taarifa muhimu za
kiuhamiaji na kuwezesha udhibiti matukio ya kihalifu.
Alisema mkoa huo ndio mapitio ya makundi ya wahamiaji haramu kutoka
Ethiopia na Somalia wanaoelekea kusini mwa Afrika, hivyo wananchi
wakitoa msaada kwa maofisa wa uhamiaji wanaweza kukomesha hali hiyo.
Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma, Koku Lwebandiza, aliishukuru serikali
kwa kuwezesha kujengwa kwa nyumba hiyo ambayo imegharimu sh milioni
434.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment