Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKATI Serikali inahangaika kutafuta masoko ya kuuzia mazao ya
wakulima, kampuni ya kizalendo ya Mkulima Malt Purpose yenye makao yake
makuu jijini Mbeya imejitosa kuanza kununua mpunga.
Kampuni hiyo ambayo kwa sasa inajishughulisha na kilimo cha mpunga
katika Kijiji cha Nambendo, wilayani Songea, Ruvuma, imejitolea kuanza
kununua mpunga wa wakulima hao kwa lengo la kuwanusuru na tatizo la
ukosefu wa soko katika msimu wa 2013/2014, ambako lengo lake ni kununua
wastani wa tani 80 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 30.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hamis
Msigwa, alisema tayari wamekwisha nunua tani 16 za mpunga.
Msigwa, alisema kampuni yake imeamua kununua mpunga huo kutokana na
wakulima wa kijiji hicho kuongeza uzalishaji wa zao hilo, kutoka
wastani wa tani 10 hadi kufikia 80 baada ya kampuni hiyo kutoa elimu
juu ya kilimo hicho, ikiwemo kuwagawia mbegu tani tatu kwa wakulima wa
vitongoji nane vya kijiji hicho pamoja na kuwalimia mshamba yao bure.
Alisema kuwa, licha ya kuwakwamua wakulima hao kwa kununua zao hilo,
kampuni hiyo inatarajia kuboresha kilimo cha zao hilo kwa kuongeza
jitihada zaidi ya kuwagawia mbegu bora ya mpunga ambayo itakuwa na
uwezo wa kuzalisha gunia 30 kwa ekari moja.
Kampuni hiyo inajishughulisha na kilimo cha zao la Mpunga katika
maeneo yafuatayo ikiwemo ,Chimala Mbeya,Mtwara vijijini pamoja na
Kijiji cha Nambendo kilichopo katika Halmashauri ya wilaya ya Songea
vijijini
mkoani Ruvuma.
mkoani Ruvuma.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment