MKURUGENZI WA VETA NYANDA ZA JUU ATEMBELEA HOSPITALI YA PERAMIHO MJINI SONGEA

Mkurugenzi wa VETA nyanda za juu,Monica Mbele akiangalia moja ya darubini katika karakana ya vifaa tiba kwenye Hospitali ya St. Joseph Peramiho,wengine ni fundi mkuu wa karakana hiyo Baraka Chumbwi kushoto na katikati kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Benedict Ngaiza. Mkurugenzi wa Mamlaka ya elimu na mafunzo (VETA) nyanda za juu,Monica Mbele akiangalia moja ya vifaa tiba vilivyoharibika katika karakana ya Hospitali ya St Joseph Peramiho,Songea vijijini.VETA ina tarajia kufundisha wataalam na mafundi wa hospitali mbalimbali kutengeza vifaa vilivyoharibika ambapo itasaidia kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kwa kuagiza au kuleta mafundi kutoka...

Tatizo La Maji Songea Sasa Latikisa Ndoo moja Lita Sh 500

Mjengwa bl...

Mafuta Yawa adimu Songea

Picha kwa hisani ya http://mwambije.blogspot.co...

HAFLA YA KUMUAGA KANAL MJENGWA DC MBINGA YAFANA SANA

Kutoka kushoto mkuu wa wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi,mkuu wa wilaya ya mbinga mstaafu Kanal Edmund Mjengwa,mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu,mkuu mpya wa wilaya Mbinga Senyi Ngaga na Mama Hanab Mwambungu wakigonga cheers wakati wa sherehe ya kumuaga Kanal Mjengwa jana mjini Mbinga. Mkuu wa zamani wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Kanal mstaafu Edmund Mjengwa akizungumza jana mjini Mbinga wakati wa sherehe yake ya kumuaga,katikati mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu na kulia mkuu mpya wa wilaya hiyo Senyi Ngaga.  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZA...

Serikali Mkoani Ruvuma imetoa mwenzi mmoja kwa Wafugaji wa ng'ombe kuhama mkoani Ruvuma

kundi kubwa la ng'ombe katika poli la hifadhi ya selousSerikali Mkoani Ruvuma imetoa mwenzi mmoja kwa Wafugaji wa jamii za Kisukuma na Wamang‘ati walioingiza Ng’ombe wao kiholela bila kufuata utaratibu kuondoka Mkoani humo vinginevyo Sheria itafuata mkondo wake ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa Oparesheni ya kuwafukuza. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said thabity Mwambungu, wakati akiongea na Viongozi wa Serikali Wilayani Tunduru kutokana ukiukwaji wa taratibu za kuingiza wanyama hao bila kufuata taratibu hali ambayo inaweza kuleta madhala na kuzuka kwa mapigano makubwa baina ya wakulima na wafugaji. Bw. Mwambungu...

SHEIKH ASHAMBULIWA, AJERUHIWA ALAZWA HOSPITALINI, VIONGOZI WA UAMSHO KIZIMBANI

Na Mwinyi Sadallah Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, Waziri Ally Chilakwechi, amepigwa na watu wasiojulikana baada ya kumvamia nyumbani kwake eneo la Mchangani mjini Tunduru na kujeruhiwa vibaya.  Sheikh Chilakwechi akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu kutoka katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru alikolazwa, alisema alishambuliwa na watu wasiojulikana juzi. Akielezea mkasa huo, alisema siku ya tukio alifuatwa na watu watatu majira ya saa 2:30 usiku nyumbani kwake wakidai kuwa kuna vurugu zimetokea katika msikiti wa Kitumbini eneo la Majengo, hivyo anahitajika kwenda kutuliza vurugu hizo. Alisema kwa kuwa alikuwa hawatambui watu hao, isingekuwa vyema kwenda huko kutokana na umbali kwa kuwa kutoka nyumbani kwake hadi kwenye msikiti huo ni zaidi...

KATIBU MKUU UN AZUNGUMZIA MPAKA WA ZIWA NYASA

Na Mwandishi wetu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki- Moon, amepongeza msimamo wa Tanzania kutafuta majawabu ya amani katika kujadiliana kuhusu mzozo wa mpaka kati yake na Malawi kwenye Ziwa Nyasa. Amesema uamuzi wa Tanzania ndiyo njia sahihi na inayokubaliwa kimataifa kutafuta na kupata suluhisho la migogoro ya namna hiyo. Ban Ki Moon ametoa pongezi hizo kwa Tanzania mjini hapa juzi wakati alipomkaribisha na kukutana kwa mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko New York, kwa ziara ya siku mbili. “Majuzi nilikutana na Rais Joyce Banda wa Malawi na akanielezea mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa na mazungumzo ambayo nchi zetu mbili zinafanya ili kupata ufumbuzi wa amani. Hii ndiyo njia sahihi na Umoja wa Mataifa unaunga mkono njia hiyo,” Ban Ki Moon...

JK: TUVUTE SUBIRA MGOGORO ZIWA NYASA

Na Mwandishi Wetu RAIS Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kuwa na subira kuhusu tatizo la mpaka wa Ziwa Nyasa. Alisema katika kushughulikia utata wa mpaka huo na nchi ya Malawi, Tume maalumu ilikuwa ikutane Septemba 10 hadi 15 mwaka huu lakini mkutano huo haukufanyika. Rais Kikwete aliyasema hayo jana katika hotuba yake ya kila mwezi kwa Watanzania na kusisitiza kuwa, nchi ya Malawi iliomba mkutano huo usogezwe mbele. “Sisi tumekubali ombi lao hivyo tunawasubili kwani subira yavuta heri, upande wetu tunaendelea na matayarisho husika kama tutaamua kwenda Mahakama ya Kimataifa (ICJ) nchini Uholanzi,” alisema. Alitoa wito kwa Watanzania kuitunza na kudumisha amani iliyopo kwa kuheshimu misingi ya katiba, kuepuka vitendo vya uvunjifu wa sheria, kuheshimiana na kuvumiliana kwa tofauti...

RC: WATENDAJI WAZEMBE WAWAJIBISHWE

na Julius Konala, Songea MKUU wa Mkoa (RC) wa Ruvuma, Said Mwambungu, amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na manispaa mkoani humo kuwawajibisha kwa kuwasimamisha kazi au kuwafukuza maofisa watendaji wa vijiji na kata wazembe ambao watashindwa kuwadhibiti watu wanaofanya uharibifu wa mazingira kwa kuchoma moto na kukata miti ovyo. Mwambungu alitoa agizo hilo jana wakati akifungua kongamano la kuweka mikakati ya kudhibiti moto hatarishi kwenye maeneo ya misitu mkoani humo lililoandaliwa na kitengo cha Misitu Uenezi, Kanda ya Kusini. Mkuu huyo wa Mkoa (RC), alisema maofisa watendaji hao wengi wao wamekuwa wakiwafumbia macho wananchi wanaojihusisha na uharibifu wa mazingira na kwamba vitendo hivyo vinahatarisha usalama wa viumbe hai na uoto wa asili ambao ni rasilimali ya taifa...

UHABA WA DAWA WAITESA SONGEA

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4 /* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-priority:99; ...

Wanajeshi Nao Watoa Maoni Katiba Mpya

Baadhi ya wapiganaji wa JWTZ Brigedi ya Kusini wakifuatilia kwa makini Mkutano wao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo(jana) katika kikosi cha JWTZ 411 KJ Songea. Picha na Mjengwa blo...

DC MSTAAFU ADAI KUTELEKEZWA

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE /* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-priority:99; mso-style-qformat:yes; ...

DC AOMBWA KUINGILIA MZOZO WA ARDHI

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4 /* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-priority:99; ...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa