Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akutana na Balozi wa Msumbiji nchini


Katibu Tawala Msaidizi wa Miundombinu Mkoa wa Ruvuma,Sevelin Tosi (kulia) akisalimiana na balozi wa msumbiji nchini,Mh. Amour Zakarius Kupela alietembelea mjini songea.Wa pili Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu.
Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania,Mh. Amour Zakarius Kupela (kushoto) akisalimiana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,Michael Kamuhanda mjini Songea jana.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (kushoto) akitoa taarifa ya mahusiano mema kati ya Tanzania na Msumbiji kwa balozi wa msumbijin nchini,Mh.Amour Kupela ofisini kwake mjini songea jana.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii,Ruvuma.
kwa hisani ya Issa Michuzi Blog

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akabidhi vyeti kwa wahitimu 502 chuo cha Ualimu Songea


 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akimpongeza mmoja kati ya wahitimu 502 wa Stashahada ya Ualimu wa Chuo cha Ualimu cha Songea mara baada ya kumkabidhi cheti chake,wakati wa mahafali ya 11 ya chuo hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akizungumza na Wazazi,Walimu na Wahitimu katika Chuo Cha Ualimu cha Songea.kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Bi. Ilolima Lugomi na kulia Mkuu wa Chuo hicho,Selemani Ubaya.
 Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Songea,Selemani Ubaya (kulia) akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu kwenda kuzungumza na kugawa vyeti kwa wahitimu 502 chuoni hapo.
 Baadhi ya Wahitimu 502 wa Chuo cha Ualimu Songea katika ngazi ya stashahada,wakimsikiliza mkuu wa chuo hicho,Selemani Ubaya (hayupo picha) wakati wa mahafari ya 11 chuoni hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Chama cha Walimu Mkoani humo,Bi. Luya Ngonyani alipowasili katika Chuo cha Ualimu cha Songea (matogoro) wakati wa mahafari chuoni hapo
Picha kwa hisani ya Michuzi Blog

Mkutano wa waendesha pikipiki Songea na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma



  Mkuu wa wilaya ya songea Roy Thomas Sabaya akitoa nasaha kwa vijana  wanaojishughulisha na kuendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali ya mjiji wa songea wakati wa mkutano kati ya vijana hao na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh Said Mwambungu  mjini Songea. Kushoto kwake ni amanda wa polisi wa mkoa huo Afande Michael Kamuhanda.
 Mkuu wa mkoa wa ruvuma Said Mwambungu akizunguza jana na vijana zaidi ya 800 wanaoendesha pikpiki katika maeneo tofauti  wilayani Songea katika mkutano wake na vijana hao uliofanyika katika ukumbi wa songea club mjin i songea,kulia ni meya wa manisopaa ya songea Charles Mhagama.
 Baadhi ya vijana wanaoendesha pikipiki mjini songea wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu hayupo pichani jana, katika ukmbi wa songea club wakati wa mkutano kati ya vijana hao na mkuu huyo wa mkoa.

Katibu wa chama cha waendesgha pikipiki wilayani Songea akiongea
Picha zote kwa Hisani ya Michuzi Blog

TAMASHA LA MAJIMAJI LA UTAMADUNI WA MKOA WA RUVUMA KUFANYIKA APRILI 27-28 MJINI SONGEA

:
Msanii wa kikundi cha ngoma za asili kutoka mkoani Ruvuma kinachoitwa Makangarawe Youth Infomation & Development Center (MYIDC) Bw. Peter Petil Komba akielezea kikapu kikapu kinachotumia kwa shughuli mbalimbali za utamaduni wa makabila ya Ruvuma wakati viongozi wa kikundi hicho walipozungumzia tamasha kubwa la Majimaji Culture Traditional Festival linalotarajiwa kufanyika kuanzia Aprili 27-28 mjini Songea, mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam leo.

Kutakua na ngoma mbalimbali pamoja na maonyesho ya tamaduni mbalimbali za makabila kuoka mkoa wa Ruvuma ambayo yataonyesha tamaduni zao kwa watu mbalimbali watakaotembelea na kuona shughuli mbalimbali za makabila hayo katika tamasha hilo.

Kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Halisi litashiriki katika tamasha hilo kwa kutoa burudani katika tamasha hilo.
Habari kwa hisani ya Full Shangwe Blog

ZIARA YA JAJI KIONGOZI MH FAKI JUNDU MKOANI RUVUMA


Jaji kiongozi wa mahakama kuu Tanzania,Mh. Faki Jundu akikata utepe kufungua mahakama ya mwanzo maposeni iliyopo wilayani songea jana,kulia ni jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya songea,Mh. Peter Chocha na kushoto hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo ya mwanzo,Aneth Senkoro.
Mkandarsi aliyejenga mahakama ya mwanzo ya maposeni wilayani songea,Efreim Malya katikati akimueleza jambo jaji kiongozi wa mahakama kuu ya tanzania,Mh. Faki Jundu wa kwanza kushoto,mara baada ya Jaji Jundu kufungua rasmi mahakama hiyo jana,kuli ni jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya songea peter Chocha.
Jaji kiongozi wa mahakama kuu Tanzania,Mh. Faki Jundu (kushoto) akipokea mti wa mparachichi kutoka kwa hakimu mkadhi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Songea Janifer Changani jana katika viwanja vya mahakama ya mwanzo maposeni songea PICHA NA MUHIDIN AMRI WA GLOBU YA JAMII.
Kwa hisani ya Issa Michuzi
Picha zaidi Bofya hapa 

Baraza la madiwani Manispaa ya Songea lakutana leo

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akisaini kitabu
cha wageni katika ofisi ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea leo kabla
ya kikao cha baraza la madiwani .
(Na Revocatus A.Kassimba wa ofisi ya mkuu wa mkoa Ruvuma)
Diwani wa Kata ya Ruvuma Mhe.Victor Ngongi akizungumza wakati wa
kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea
kilichoketi kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka 2012/2012 hivi leo
Msafara wa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Charles
Mhagama ukielekea katika ukumbi wa mikutano tayari kwa kikao cha
kupitisha bajeti ya mwaka 2012/2013.

Picha na Full Shangwe Blog

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AZUNGUMZA NA WANAKIJIJI WA KIJIJI CHA MTUNDUWALO



 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akizungumza  leo na wananchi wa kijiji cha Mtunduwalo kata ya Luanda wilaya ya Mbinga kufuatia malalmiko yao ya kulipwa fidia isiyolingana na thamani ya eneo waliloachia kupisha mradi wa mgodi wa Makaa ya Mawe Ngaka.
 Mmoja wa wanakijiji Mtunduwalo John Nyimbo akitoa maelezo juu ya malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma (hayupo pichani) kuhusu kulipwa fidia kidogo ya ardhi waliyoitoa kupisha mradi wa mgodi wa makaa ya mawe Ngaka wilayani Mbinga.
 Mkuu wa Mkoa waRuvuma Said Mwambungu akiagana na wanakijiji cha Mtunduwalo baada ya kumalizika kwa mkutan.
Wananchi wa kijiji cha Mtunduwalo katika Kata ya Luanda wilaya ya Mbinga wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma (hayupo pichani) kuhusu malalamiko ya kulipwa fidia pungufu ya maeneo yao kupisha mradi wa makaa ya mawe Ngaka hivi le.
Picha na Revocatus Kassimba, Afisa Habari-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa