Home » » TAMASHA LA MAJIMAJI LA UTAMADUNI WA MKOA WA RUVUMA KUFANYIKA APRILI 27-28 MJINI SONGEA

TAMASHA LA MAJIMAJI LA UTAMADUNI WA MKOA WA RUVUMA KUFANYIKA APRILI 27-28 MJINI SONGEA

:
Msanii wa kikundi cha ngoma za asili kutoka mkoani Ruvuma kinachoitwa Makangarawe Youth Infomation & Development Center (MYIDC) Bw. Peter Petil Komba akielezea kikapu kikapu kinachotumia kwa shughuli mbalimbali za utamaduni wa makabila ya Ruvuma wakati viongozi wa kikundi hicho walipozungumzia tamasha kubwa la Majimaji Culture Traditional Festival linalotarajiwa kufanyika kuanzia Aprili 27-28 mjini Songea, mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam leo.

Kutakua na ngoma mbalimbali pamoja na maonyesho ya tamaduni mbalimbali za makabila kuoka mkoa wa Ruvuma ambayo yataonyesha tamaduni zao kwa watu mbalimbali watakaotembelea na kuona shughuli mbalimbali za makabila hayo katika tamasha hilo.

Kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Halisi litashiriki katika tamasha hilo kwa kutoa burudani katika tamasha hilo.
Habari kwa hisani ya Full Shangwe Blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa