UMOJA
wa wakazi wa wilaya mpya ya Nyasa, mkoani Ruvuma, waishio jijini Dar es
salaam, umetoa msaada wa boti moja yenye thamani ya sh milioni 16 kwa
wananchi wa Mbambabay wilayani humo kwa ajili ya kuendeshea shughuli za
uvuvi wa kisasa.
Boti
hiyo ilikabidhiwa mwishoni mwa wiki na mwenyekiti wa umoja huo Cassian
Njowoka, kwa mkuu wa wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi ili litolewe kwa
kikundi kimojawapo ambacho kinajishughulisha na shughuli ya uvuvi kwa
madai kwamba mapato yatakayopatikana yaweze kununulia boti nyingine
ambayo itagawiwa kwa kikundi kingine.
Njowoka
alisema kuwa lengo la chama chao ni kuhakikisha kila kikundi cha uvuvi
kinapata boti ya kisasa kwa lengo la kuongeza ufanisi katika shughuli
zao tofauti na ilivyo sasa ambapo wanaendesha uvuvi wa hatari wa kutumia
mitumbwi...
POLISI RUVUMA WAKAMATA MENO YA TEMBO WILAYANI TUNDURU
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki akiangalia pembe zilizokamatwa——————————————–JESHI
la polisi mkoani Ruvuma kwa mara nyingine limefanikiwa kukamata nyara
za serikali katika wilaya ya Tunduru tukio ambalo limetokea Julai 21
mwaka huu majira ya saa 11:40 alfajiri lililotanguliwa na tukio jingine
lililotokea Juni 26 mwaka huu ambapo jumla ya meno 18 ya tembo
yalikamatwa wilayani humo kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na idara ya
wanyamapori pamoja na wananchi wanaotoa taarifa za siri kwa vyombo
hivyo vya ulinzi na usalama.Akizungumza na...
SHUJAA WA TANZANIA ALIYEFIA DARFUR RODNEY NDUNGURU AZIKWA KWAO SONGEA
Asikari wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Rodney Ndunguru
Aliye kaa katikati ni mama wa marehemu Rodney Ndunguru
Askari wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Rodney Ndunguru wakati wakielekea katika makaburi ya Mjimwema
Umati wa watu uliojitokeza katika mazishi ya Rodney Ndunguru katika makaburi ya mjimwema jana
Mwili wa Rodney Ndunguru ukiingizwa katika kaburi
Mama wa marehemu Rodney Ndunguru akiweka taji katika kaburi la mwanaye---------------------------------------
Na Cresensia Kapinga,Songea.
SIMANZI
,Vilio,majonzi vimetawala wakati wa mazishi...
Barabara ya Songea, Tunduru-Mtwara kuanza kujengwa
MKOA wa Ruvuma utakuwa na fursa nyingi za kiuchumi na
maendeleo mara baada ya kufunguka kwamtandao wa barabara ndani yakipindi kifupi
kijacho ambapo kilometa 1,500 za kutoka Songea, Tunduru hadi Mtwara
zitakuwa zimejengwa kwa kiwango cha lami kwa kipindi cha kuanza mwaka huu
wafedha wa 2013/14.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Mizengo Pinda
wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,katika
mkutano wahadhara wakati akiwa katika ziara ya siku nane ya kukagua shughuli za
maendeleo za mkoa huo.
Pinda amesema kwasasa mkoa huo unamiradi mingi ya barabara ambayo ipo katika hatuaza
mwisho za upembuzi wa kina na hivyo muda si mrefu ujezi wa barabara hizo utaanza.
Amesema barabaraya Songea hadi Namtumbo ambayo ni ya kilometa 73 kwa...
OCD MBINGA ALALAMIKIWA NA ASKARI

Na Muhidin Amri–Mbinga
BAADHI
ya askari polisi wa kituo kikuu Mbinga mjini,wamemtuhumu mkuu wa
polisi wa wilaya hiyo(OCD)Jastine Joseph kuwa ni mtu anayetumia madaraka
yake vibaya kwa kuendesha manyanyaso dhidi ya askari wa vyeo vya chini
na kumuomba Mkuu wa jeshi ilo Said Mwema kumuondoa haraka kabla ya hali
haijawa mbaya zaidi.
Wakizungumza
na mtandao huu kwa masharti ya kutotajwa majina yao,askari hao
wamelalamika kuwa OCD wao amekuwa akitoa lugha za dharau na hata
zisizopendeza kwao hali inayowavunja moyo wa kazi askari wengine katika
wilaya...
Dawa ya waharibifu wa mazingira Ruvuma imeiva
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema mtu yoyote atakaye
haribu vyanzo vya maji au kutumia Maji ovyo hatua za kisheria zitachukuliwa
dhidi yake.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu ameya sema hayo wakati
wadau mbalimbali wa Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini kujadili jinsi
ya kukabiliana na Majanga yanayo sababisha kiwango cha maji kushuka.
Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Said Thabiti Mwambungu amesema kiwango cha uharibifu wa mazingira katika
mkoa wa Ruvuma una zidi kuongezeka kwa watu kilima katika vyanzo vya maji
pamoja na kutumia maji bila kibali cha Maafisa wa Bonde la mto Ruvuma , watu
hao wakibainika wata kamatwa na kufikishwa kwenye vyombo kisheria
Afisa wa Maji
Katika Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya
Kusini. Masaru Razaro Msengi amesma...
Vijana watakiwa kuendelezwa
Na Amon Mtega, Songea
VIJANA wanatakiwa kuendelezwa katika fani zao za kitaaluma na
shughuli wanazopenda kuzifanya katika maisha yao ili waweze kujipatia
maendeleo. Wito huo, umetolewa jana na Mratibu wa Mradi wa Shirila la
Resteless Development mkoani Ruvuma, wakati akiwakaribisha vijana kutoka
vyuo mbalimbali kwenye mdahalo uliyoandaliwa na shirika hilo huku.
Mdahalo huo, ulikuwa na mada ya vijana wanajitambuaje na wasaidiwaje
ili waweze kukabiliana na changamoto zinazo wakabili katika maisha yao.Alisema
ili vijana waweze kumudu kukabiliana na changamoto zinazowakabili
katika maisha, ni lazima sekta za umma na za watu binafsi ziweze kutoa
misaada ya kielimu ya kukabiliana na changamoto hizo.Alisema
kufuatia shirika hilo ambalo linafanya...
Watoto Ruvuma waomba kutunzwa
WATOTO mkoani Ruvuma wanaoishi katika mazingira magumu wametoa wito kwa kampuni na jamii kutowasahau kutunzwa na kuwatembelea. Kauli hiyo waliitoa mjini hapa hivi karibuni katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2013 baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania.
Watoto hao waliomba wadau kuiga mfano wa Vodacom Tanzania kwa kuwa itakuwa changamoto kwao kuweza kutimiza yale yanayotarajiwa kutoka kwao na hatimaye kuwa Watanzania wenye ari ya kuleta maendeleo na mafanikio chanya katika Taifa.
Wafanyakazi hao walifika hapo kwa lengo la kuwaona na kuwafariji na kutoa msaada wa kilo 100 za mahindi, sabuni na mafuta ya kujipaka pamoja na viburudisho kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho chenye watoto 64.
Akizungumza katika makabidhiano ya msaada hiyo, Meneja...