Home » » Watoto Ruvuma waomba kutunzwa

Watoto Ruvuma waomba kutunzwa

WATOTO mkoani Ruvuma wanaoishi katika mazingira magumu wametoa wito kwa kampuni na jamii kutowasahau kutunzwa na kuwatembelea. Kauli hiyo waliitoa mjini hapa hivi karibuni katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2013 baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania.


Watoto hao waliomba wadau kuiga mfano wa Vodacom Tanzania kwa kuwa itakuwa changamoto kwao kuweza kutimiza yale yanayotarajiwa kutoka kwao na hatimaye kuwa Watanzania wenye ari ya kuleta maendeleo na mafanikio chanya katika Taifa.

Wafanyakazi hao walifika hapo kwa lengo la kuwaona na kuwafariji na kutoa msaada wa kilo 100 za mahindi, sabuni na mafuta ya kujipaka pamoja na viburudisho kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho chenye watoto 64.

Akizungumza katika makabidhiano ya msaada hiyo, Meneja wa Vodacom Ruvuma, Michael Kipuyo, alisema wameona ni kipindi kizuri kuwakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa ajili ya kuwasaidia nao wajisikie ni sehemu ya jamii inawajali.

“Vodacom tunajali wateja wetu wa sasa na wale wa baadaye kwa kuwa kwa kusaidia watoto hawa tunasaidia jamii na Serikali kulea watoto watakaouja kuwa ni nguvu kazi ya Taifa hapo baadaye katika mazingira ya amani na hatimaye kuwafanya wajisikie kuwa ni sehemu ya jamii,” alisema Kipuyo.

Watoto hao waliwashukuru wafanyakazi hao kwa kuwakumbuka katika kipindi hiki ambapo Afrika inaadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika na kuwakumbuka wale waliofariki katika kudai haki zao kule Afrika ya Kusini mwaka 1976.

Waliomba wadau kuiga mfano wa Vodacom Tanzania kwa kuwa itakuwa changamoto kuwa Watanzania wenye ari ya kuleta maendeleo na mafanikio chanya katika Taifa.

CHANZO: GAZETI LA MTANZANIA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa