Home » » Vijana watakiwa kuendelezwa

Vijana watakiwa kuendelezwa

VIJANA wanatakiwa kuendelezwa katika fani zao za kitaaluma na shughuli wanazopenda kuzifanya katika maisha yao ili waweze kujipatia maendeleo. Wito huo, umetolewa jana na Mratibu wa Mradi wa Shirila la Resteless Development mkoani Ruvuma, wakati akiwakaribisha vijana kutoka vyuo mbalimbali kwenye mdahalo uliyoandaliwa na shirika hilo huku.
Mdahalo huo, ulikuwa na mada ya vijana wanajitambuaje na wasaidiwaje ili waweze kukabiliana na changamoto zinazo wakabili katika maisha yao.

Alisema ili vijana waweze kumudu kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika maisha, ni lazima sekta za umma na za watu binafsi ziweze kutoa misaada ya kielimu ya kukabiliana na changamoto hizo.

Alisema kufuatia shirika hilo ambalo linafanya kazi na vijana katika nchi 11 ulimwenguni,limebaini vijana wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa za upande wa ajira, pindi wanapohitimu elimu zao.

Kwa upande wa watoa mada, Lawrence Ambokile alisema vijana wengi wanakata tamaa maisha kwa sababu hawajapewa elimu ya kujitambua.

Alisema jamii, inawategemea vijana kutoka vyuo vikuu hivyo inatakiwa iwalinde na kuwapa mawazo mazuri ambayo yatakuwa msingi wa maisha yao.

CHANZO: MTANZANIA GAZETI

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa