Asikari wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Rodney Ndunguru
Aliye kaa katikati ni mama wa marehemu Rodney Ndunguru
Askari wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Rodney Ndunguru wakati wakielekea katika makaburi ya Mjimwema
Mwili wa Rodney Ndunguru ukiingizwa katika kaburi
Mama wa marehemu Rodney Ndunguru akiweka taji katika kaburi la mwanaye
------------------------------ ---------
------------------------------
Na Cresensia Kapinga,Songea.
SIMANZI
,Vilio,majonzi vimetawala wakati wa mazishi ya askari wa Jeshi la
Wananchi Rodney Ndunguru wa kikosi cha makomando cha 92 KJ Ngerengere
mkoani Morogoro ambapo mamia ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwemo askari
wa Jeshi la wananchi ambao walihudhuria mazishi yaliyofanyika jana
kwenye makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea.
Katika
mazishi hayo ambayo yaliongozwa na Paroko wa kanisa katoriki jimbo kuu
la Songea parokia ya Mjimwema padre Noel Duwe ambaye wakati akiendesha
ibada ya mazishi aliwaonya Watanzania kutochezea amani na kwamba
utulivu walionao watanzania unahitajika kulindwa kwa namna ya aina
yeyote na si vinginevyo.
Padre
Due alisema kuwa kwa wale wote wanaotaka kuchezea amani na utulivu
tulionao wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa kuwa watanzania
hatujazoea vurugu wala umwagaji wa damu jambo ambalo lilionekana kuvuta
hisia kwa watu waliofika kuomboleza msiba hu.
Aidha
Padri Due alimfagilia waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano Mizengo Pinda
kwa kauli yake aliyoitoa Bungeni kuwa kuwa jeshi la Polisi lihakikishe
kuwa linawadhibiti watu wanaoleta fujo kwa kupiga na kwamba kauli yenye
agizo hilo inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote badala ya kuibeza kwa
kuwa hivi sasa watu wengi wamekuwa wakidharau vyombo vya Dola wakizani
kuwa serikali haipo.
Kwa
upande wake Kaimu wa Brigedi ya kanda ya kusini Kanari George Msongole
alieleza kuwa taarifa ya kifo cha Rodney ilipokelewa muda mfupi baada
ya kifo chake na kuwa Jeshi la wananachi linaungana na familia ya
marehemu katika majonzi na msiba mzito.
Kwa
upande wake msemaji wa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru amesema
kuwa familia imepata pengo kubwa kwa kuondokewa na kijana wao ,na
ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuisaidia ili waweze kujengewa
nyumba ambayo itwasaidia kwa kuishi mama yake mzazi na mjane.
Alisema
kuwa Rodney Ndunguru amefariki akiwa na miaka takribani miaka saba
kazini na akiwa na umri wa miaka 28 ambapo kimsingi kifo chake kimeacha
pengo kubwa katika famila kwani katika uhai wake ilikuwa farja kwa ndugu
na jamaa.
Rodney
Ndungu amezikwa saa 10:45 jioni kwenye makaburi ya mjimwema ambako
mamia ya wakazi ya mkoa wa Ruvuma walihudhulia akiwemo mwakilishi wa
mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu ambaye ni katibu tawala ya wilaya ya
songea Joseph Kapinga na kwamba mazishi yaliendeshwa kijeshi ambapo
askari wote walikuwa wamevaa sare huku wakifunga vitambaa vyeusi kwenye
mikono yao.
habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment