Na Muhidin Amri–Mbinga
BAADHI
ya askari polisi wa kituo kikuu Mbinga mjini,wamemtuhumu mkuu wa
polisi wa wilaya hiyo(OCD)Jastine Joseph kuwa ni mtu anayetumia madaraka
yake vibaya kwa kuendesha manyanyaso dhidi ya askari wa vyeo vya chini
na kumuomba Mkuu wa jeshi ilo Said Mwema kumuondoa haraka kabla ya hali
haijawa mbaya zaidi.
Wakizungumza
na mtandao huu kwa masharti ya kutotajwa majina yao,askari hao
wamelalamika kuwa OCD wao amekuwa akitoa lugha za dharau na hata
zisizopendeza kwao hali inayowavunja moyo wa kazi askari wengine katika
wilaya hiyo.
Walisema,iwapo
jeshi litashindwa kumuhamisha Jastine kunaweza kutokea maafa makubwa
kwani hawatoweza kuvumilia vitendo vinavyofanywa na afisa huyo hasa
ukizingatia kuwa na wao ni watu wakubwa tena wenye familia kama yeye
hivyo kitendo cha kuwatolea lugha za kiuni ni sawa na kuwadhalilisha.
Aidha
wameshauri hata maafisa wengine katika wilaya hiyo wanatakiwa kuondoka
kwani wameshaaka Mbinga kwa muda mrefu hivyo ni vema kupelekwa katika
maeneo mengine ya nchi ili wakapate changamoto mpya za utendaji wa kazi,
na kuendelea kuwepo katika wilaya hiyo ni tatizo kubwa kwani
wameshafahamika na watu wengine hali inayowafanya kushindwa kuchukua
maamuzi sahihi.
Wamesema
ocd wao ni mtu hasiyetaka ushauri kutoka kwa mwingine hata kwa maafisa
wenzake jambo linalomfanya kutengwa na kujikuta na yuko pekee yake au na
wale askari wa kabila lake tu jambo lililowafanya askari kuwepo katika
makundi hasa baada ya kufika Jastine kitu ambacho siku za nyuma
hakikuwepo na askari wote walikuwa ndugu moja wakiishi na kusaidiana
tofauti na sasa.
“huyu
mkuu wetu ni tatizo kubwa,sijui hata mtu aliyempendekeza kuwa OCD
ametumia kigezo gani,hafai kabisa yeye kazi yake ni majungu tu na sio
vinginevyo”alisema mmoja wa askari hao.
Kwa
upande wake Jastine alikanusha tuhuma hizo na kuziita kuwa ni unafiki
unaofanywa na askari wachache waliozoea kula rushwa kila mara hasa kwa
waendesha pikipiki jambo ambalo yeye hataki kusikia katika uongozi wake.
“hizo
tuhuma sio za kweli,zinafanywa na baadhi ya askari wngu hasa wale wala
rushwa,nimeshaelekeza wakikamata pikipiki waje na faini hapa au mmiliki
wake sio kuleta pikipiki hatuna eneo la kupaki kwani hizi tulizonazo ni
nyingi na hatuna sehemu ya kuzipeleka”alisema.
Naye
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki alikiri kuwepo kwa
malalamiko ya askari wa vyeo vya chini dhidi ya OCDwao na kuhaidia kuwa
atashughulikia tuhuma hizo ili kupata ukweli wa jambo ilo.
“sisi
hatufanyi mambo kwa kukurupuka tu lazima tufanye uchunguzi ili
tujiridhishe,unajua ukishakuwa kiongozi unatakiwa kuwa makini hasa
katika maamuzi ili usifanye mambo kwa kumuonea mtu lazima utende haki
kila wakati”alisema RPC
0 comments:
Post a Comment