WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa mwezi mmoja Ofi sa Ardhi wa wilaya
ya Namtumbo, mkoani Ruvuma, Maurus Yera awe ametafuta ardhi ya kuwafi
dia wakazi 21 wa kijiji cha Lwinga wilayani humo ambao eneo lao lenye
ukubwa wa ekari 101 lilitwaliwa na serikali mwaka 2008.
Eneo hilo lilitwaliwa kupisha ujenzi wa shule ya sekondari ya mkoa wa
Ruvuma. Alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa
wananchi hao kupitia mabango, ambapo walimuomba awatatulie kero hiyo ya
madai ya fidia ya ardhi iliyodumu kwa miaka 10 bila kupatiwa ufumbuzi.
Waziri Mkuu alisema haoni sababu ya Halmashauri hiyo kushindwa
kuwafidia wananchi hao sehemu ya ardhi kwa muda wote huo ukizingatia
wilaya hiyo ina hifadhi ya ardhi.
“Nataka wananchi hawa wawe wamelipwa fidia yao ya ardhi kabla ya siku
kuu ya Krismasi ya mwaka huu. Serikali haiko tayari kuona wananchi wake
waliotoa ardhi kupisha maendeleo wakisumbuliwa,” alisema.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment