Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (wa kwanza kulia) akikagua sehemu ya mtambo wa kutibu na kusafisha maji wa Matogoro, pamoja na Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Songea (SOUWASA), Mhandisi John Kapinga.
Mtambo wa kutibu na kusafisha maji wa Matogoro, Songea Mjini, mkoani Ruvuma
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (SOUWASA), Mhandisi Patrick Kibasa katika eneo la Misufini.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akishuka baada ya kukagua tanki la mradi wa Mtendewawa, wilayani Songea Mjini, mkoa wa Ruvuma.
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesisitiza kuwa wizara yake
haitakuwa kikwazo cha utekelezaji wa ahadi ya Rais, Dkt. John Magufuli
ya kuwapatia wananchi majisafi na salama, bali itasimimamia utekelezaji
wa miradi hiyo ipasavyo ili ikamilike kwa wakati na kuleta tija.
Aweso
alizungumza hayo katika ziara yake ya kikazi aliyoianza katika mkoa wa
Ruvuma, ambapo anakagua utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya zote
mkoani humo.
‘‘Niwahakikishieni
wizara haitakuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini,
zaidi ya kuhakikisha miradi yote tunayoitekeleza inaleta tija na
kumaliza kero ya maji kwa wananchi kulingana na maagizo ya Rais. Hivyo,
lazima fedha zifike kwa wakati na zitumike kwa usahihi ili miradi yote
ikamilike kwa wakati kulingana na mikataba,’’ alisema Naibu Waziri.
‘‘Ni
jukumu langu kusimamia hilo na ninawaagiza watendaji wote wasimamie
miradi yote hatua kwa hatua na watoe taarifa sahihi za maendeleo yake,
ili sisi viongozi tujue changamoto na kutoa msukumo katika kufanikisha
miradi hiyo itakayokuwa na tija na thamani halisi ya fedha
zinazotumika,’’alisisitiza Aweso.
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ametoa pongezi kwa SOUWASA kwa usimamizi
mzuri wa miradi na hatua inazozichukua kwa nia ya kumaliza kero ya maji
katika maeneo ya mji huo kama Midizini na Misufini ambayo yalikuwa na
kero kubwa, lakini kwa sasa wananchi kukiri kupata huduma hiyo.
Katika
ziara hiyo ameanza kwa kutembelea Wilaya ya Songea, ambapo ametembelea
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Songea (SOUWASA) na
kuweza kuzungumza na menejimenti yake, pamoja na watumishi.
Aidha,
alitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya hiyo ikiwemo
eneo la mradi wa Bwawa la Luhira, mtambo wa kutibu na kusafishia maji
wa Matogoro, mradi wa upanuzi wa mtandao wa majisafi Songea.
0 comments:
Post a Comment