KAMATI
ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imezipitisha
kampuni 12 kuchuana katika ununuzi wa korosho za wakulima zikiwa ni
juhudi za Serikali kuwaondolea kero hiyo.
Pamoja
na maamuzi hayo, pia Kamati hiyo imetakiwa kuwalipa wakulima Sh 1,100
au zaidi kwa kilo moja na kwamba mfumo huo hautaruhusu utaratibu wa
kuwakopa wakulima hao kuanzia Novemba 22 mwaka huu.
Akitangaza
maamuzi hayo, Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa
Wilaya ya Tunduru, Chande Nalicho alisema maamuzi hayo yamefikiwa katika
kikao kilichoketi Novemba 21 mwaka huu.
Nalicho
amewatahadharisha walanguzi walionunua korosho hizo kutoka kwa wakulima
kwa kupitia vipimo haramu vya kangomba kuwa hawatapewa mwanya wa kuuza
wala kusafirishaa korosho hizo kutoka nje ya wilaya hiyo na kwamba
atakayenaswa Sheria itafuata mkondo wake.
Katika
taarifa hiyo, Nalicho alizitaja kampuni hizo kuwa ni Export Trading Co.
Limited, Prayosa, Kulaathool Co. Ltd, Shareeji Impex Ltd, Saidi Mohamed
Said pamoja na Kampuni Kongwe ya Olam Tanzania Ltd.
Nyingine
ni China Pesticide Tanzania Ltd, Amina Seti, Saweya Impex Tanzania Ltd,
Alpha Choice Ltd, Sunrise Commodities pamoja na Chama Kikuu cha
Ushirika cha Wakulima wa korosho Wilayani Tunduru (TAMCU Ltd).
Chanzo;Habari Leo
0 comments:
Post a Comment