JIBU LA SWALI LA MBUNGE Namtumbo
SERIKALI imetakiwa kutoa kazi kwa makandarasi ambao wameonyesha
uwezo katika kutekeleza kazi zao na kukamilisha miradi ya ujenzi wa
barabara ya kutoka Songea –Mbinga na kutoka Mbinga – Songea kwa wakati
na kuachana na makandarasi wababaishaji ambao wamekuwa wakiisumbua
serikali.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni mjini hapa na Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa (CCM), wakati alipokuwa akiuliza swali la msingi.
Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua ni lini mkandarasi
mwingine atapatikana ili kazi ya ujenzi wa barabara hiyo uweze
kukamilika kama ilivyokusudiwa.
“Serikali ilimsimamisha mkandarasi wa barabara ya Namtumbo-Tunduru
kutokana na kutofanya kazi yake inavyotakiwa kwa mujibu wa mkataba,”
alisema mbunge huyo.
Akijibu maswali hayo kwa pamoja Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi
Gerson Lwenge, amekiri mkandarasi wa ujenzi wa barabara ya
Namtumbo-Tunduru kuwa ilifika mahali akaonekana ni mbabaishaji, hivyo
kusimamishwa.
Aidha, alitoa wito kwa makandarasi ambao wana uwezo kujitokeza na
kuomba tenda mara tu zinapotangazwa ili waweze kupewa kazi hizo kwa
kuwa tayari kazi yao ya awali itakuwa imeonekana.
Naibu waziri huyo alisema suala la kuomba tenda ni utaratibu ambao
upo na unatakiwa kufuatwa na makandarasi wote. Alisema mchakato wa
kuwapata makandarasi wengine kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa
barabara ya Namtumbo –Tunduru kwa kiwango cha lami unaendelea.
Alifafanua kuwa tenda ya ujenzi wa barabara hiyo ilitangazwa Septemba
1, 2013, na kuongeza kuwa wazabuni walitembelea barabara hiyo Septemba
19, 2013 ili waweze kujaza zabuni zao.
Lwenge alieleza kuwa zabuni hizo zilifungwa Novemba 12, 2013 ili kazi
ya kutathmini ianze, lengo likiwa ni kuwapata makandarasi mapema
iwezekanavyo.
chanzo;tanzania daima
0 comments:
Post a Comment